Wimbo Ulio Bora Mlango 6 Song Of Songs
Wimbo Ulio Bora 6:1 SongOfSongs 6:1
Mpendwa wako amekwenda wapi, Wewe uliye mzuri katika wanawake? Mpendwa wako amegeukia upande upi, Ili tumtafute pamoja nawe?
Wimbo Ulio Bora 6:2 SongOfSongs 6:2
Mpendwa wangu ameshukia bustani yake, Kwenye matuta ya rihani; Ili kulisha penye bustani, Ili kuchuma nyinyoro.
Wimbo Ulio Bora 6:3 SongOfSongs 6:3
Mimi ni wake mpendwa wangu, naye ni wangu, Hulisha kundi lake penye nyinyoro.
Wimbo Ulio Bora 6:4 SongOfSongs 6:4
Mpenzi wangu, u mzuri kama Tirza, Mwenye kupendeza kama Yerusalemu, Wa kutisha kama wenye bendera.
Wimbo Ulio Bora 6:5 SongOfSongs 6:5
Uyageuzie macho yako mbali nami, Kwa maana yamenitisha sana. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, Wakijilaza mbavuni pa Gileadi.
Wimbo Ulio Bora 6:6 SongOfSongs 6:6
Meno yako kama kundi la kondoo, Wakipanda kutoka kuoshwa; Ambao kila mmoja amezaa mapacha, Wala hakuna aliyefiwa kati yao.
Wimbo Ulio Bora 6:7 SongOfSongs 6:7
Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga, Nyuma ya barakoa yako.
Wimbo Ulio Bora 6:8 SongOfSongs 6:8
Wako malkia sitini, na masuria themanini, Na wanawali wasiohesabika;
Wimbo Ulio Bora 6:9 SongOfSongs 6:9
Hua wangu, mkamilifu wangu, ni mmoja tu, Mtoto wa pekee wa mamaye. Ndiye kipenzi chake aliyemzaa, Binti wakamwona wakamwita heri; Malkia na masuria nao wakamwona, Wakamsifu, wakisema,
Wimbo Ulio Bora 6:10 SongOfSongs 6:10
Ni nani huyu atazamaye kama alfajiri, Mzuri kama mwezi, safi kama jua, Wa kutisha kama wenye bendera?
Wimbo Ulio Bora 6:11 SongOfSongs 6:11
Nalishukia bustani ya milozi, Ili kuyatazama machipuko ya bondeni; Nione kama mzabibu umechanua, Kama mikomamanga imetoa maua.
Wimbo Ulio Bora 6:12 SongOfSongs 6:12
Kabla sijajua, roho yangu ilinileta Katikati ya magari ya wakuu wangu.
Wimbo Ulio Bora 6:13 SongOfSongs 6:13
Rudi, rudi, Mshulami, Rudi, rudi, ili sisi tukutazame.