Wimbo Ulio Bora Mlango 3 Song Of Songs

Wimbo Ulio Bora 3:1 SongOfSongs 3:1

Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nalimtafuta, nisimpate.

Wimbo Ulio Bora 3:2 SongOfSongs 3:2

Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani, Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate.

Wimbo Ulio Bora 3:3 SongOfSongs 3:3

Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?

Wimbo Ulio Bora 3:4 SongOfSongs 3:4

Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa.

Wimbo Ulio Bora 3:5 SongOfSongs 3:5

Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.

Wimbo Ulio Bora 3:6 SongOfSongs 3:6

Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?

Wimbo Ulio Bora 3:7 SongOfSongs 3:7

Tazama, ni machela yake Sulemani; Mashujaa sitini waizunguka, Wa mashujaa wa Israeli.

Wimbo Ulio Bora 3:8 SongOfSongs 3:8

Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya kamsa za usiku.

Wimbo Ulio Bora 3:9 SongOfSongs 3:9

Mfalme Sulemani alijifanyizia machela Ya miti ya Lebanoni;

Wimbo Ulio Bora 3:10 SongOfSongs 3:10

Nguzo zake alizifanyiza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, Gari lake limenakishiwa njumu, Hiba ya binti za Yerusalemu.

Wimbo Ulio Bora 3:11 SongOfSongs 3:11

Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alivyovikwa na mamaye, Siku ya maposo yake, Siku ya furaha ya moyo wake.