Wimbo Ulio Bora Mlango 5 Song Of Songs

Wimbo Ulio Bora 5:1 SongOfSongs 5:1

Naingia bustanini mwangu, umbu langu, bibi arusi, Nachuma manemane yangu na rihani, Nala sega la asali na asali yangu, Nanywa divai yangu na maziwa. Kaleni, rafiki zangu, kanyweni, Naam, nyweni sana, wapendwa wangu.

Wimbo Ulio Bora 5:2 SongOfSongs 5:2

Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.

Wimbo Ulio Bora 5:3 SongOfSongs 5:3

Nimeivua kanzu yangu; niivaeje? Nimeitawadha miguu; niichafueje?

Wimbo Ulio Bora 5:4 SongOfSongs 5:4

Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni, Na moyo wangu ukachomeka kwa ajili yake.

Wimbo Ulio Bora 5:5 SongOfSongs 5:5

Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu; Mikono yangu ilidondoza manemane, Na vidole vyangu matone ya manemane, Penye vipini vya komeo.

Wimbo Ulio Bora 5:6 SongOfSongs 5:6

Nalimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita; (Nimezimia nafsi yangu aliponena), Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie.

Wimbo Ulio Bora 5:7 SongOfSongs 5:7

Walinzi wazungukao mjini waliniona, Wakanipiga na kunitia jeraha, Walinzi walindao kuta zake Wakaninyang'anya shela yangu.

Wimbo Ulio Bora 5:8 SongOfSongs 5:8

Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Ninyi mkimwona mpendwa wangu, Ni nini mtakayomwambia? Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.

Wimbo Ulio Bora 5:9 SongOfSongs 5:9

Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako, Wewe uliye mzuri katika wanawake, Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako, Hata wewe utusihi hivyo?

Wimbo Ulio Bora 5:10 SongOfSongs 5:10

Mpendwa wangu ni mweupe, tena mwekundu, Mashuhuri miongoni mwa elfu kumi;

Wimbo Ulio Bora 5:11 SongOfSongs 5:11

Kichwa chake ni kama dhahabu safi sana, Nywele zake ni za ukoka, nyeusi kama kunguru;

Wimbo Ulio Bora 5:12 SongOfSongs 5:12

Macho yake ni kama hua penye vijito, Wakioga kwa maziwa, wakiikalia mito iliyojaa;

Wimbo Ulio Bora 5:13 SongOfSongs 5:13

Mashavu yake ni kama matuta ya rihani, Ambayo hufanyizwa manukato; Midomo yake ni kama nyinyoro, Inadondoza matone ya manemane;

Wimbo Ulio Bora 5:14 SongOfSongs 5:14

Mikono yake ni kama mianzi ya dhahabu, lliyopambwa kwa zabarajadi; Kiwiliwili chake kama kazi ya pembe, Iliyonakishiwa kwa yakuti samawi;

Wimbo Ulio Bora 5:15 SongOfSongs 5:15

Miguu yake ni kama nguzo za marimari, Zilizowekwa juu ya misingi ya dhahabu; Sura yake ni kama Lebanoni, Ni bora mfano wa mierezi;

Wimbo Ulio Bora 5:16 SongOfSongs 5:16

Kinywa chake kimejaa maneno matamu, Ndiye mzuri sana pia pia. Ni huyu mpendwa wangu, ni huyu rafiki yangu, Enyi binti za Yerusalemu.