26 Yesu Unipendaye

By Angela Chibalonza

Lyrics

Yesu unipendaye Kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye, 
Mwovu akinijia; Yafiche ubavuni, Mwako maisha yangu; 
Nifiikishe mbinguni Wokoe moyo wangu.

Ngome nyingine sina; Nategemea kwako.
Usinitupe Bwana, Nipe neema yako, 
Ninakuamania Mwenye kuniwezesha; 
Shari wanikingia, Vitani wanitosha.

Nakutaka Mpaji Vyote napata kwako; 
Niwapo muhitaji, Utanijazi vyako; 
Nao waangukao Wanyonge wape nguvu; 
Poza wauguao, Uongoze vipofu.

Bwana umeniosha Moyo kwa damu yako; 
Neema ya kutosha Yapatikana kwako; 
Kwako Bwana naona Kisima cha uzima; 
Mwangu moyoni Bwana, Bubujika daima.