Hakuna Kama Wewe Lyrics

By Anthony Musembi

Lyrics

Mbingu na dunia zinakuinamia 

Mbingu na dunia zinakutambua 

Mbingu na dunia zinakusujudia 


Hakuna kama wewe 

Hakuna kama wewe 

Hakuna kama wewe Baba 


Wazee ishirini na wanne 

Tangu mwanzo wa jadi hata milele 

Wanainama mbele zako 

Mtakatifu mtakatifu 


Ndege angani wanakujua 

Samaki baharini wanakutambua 

Wanyama wa porini na pia wanakuelewa 

Mimi ni nani nisikuabudu 


Hakuna kama wewe 

Hakuna kama wewe 

Hakuna kama wewe Baba 


Sio masomo yetu 

Sio hekima yetu 

Sio sayansi wala filosofia 

Sio biashara tunazofanya 

Usiku na mchana 

Sio bidii wala dini 

Sio pesa wala mali ya dunia 

Bali ni kwa nguvu zako 


Hakuna kama wewe 

Hakuna kama wewe 

Hakuna kama wewe Baba 


Yote ni wewe Baba umenitendea 

Sina kitu naweza jiringia 

Vyote ni vyako, vyote ni vyako Baba 


Hewa ninayo vuta 

Maisha ninayo ishi 

Bila wewe siwezi 


Hakuna kama wewe 

Hakuna kama wewe 

Hakuna kama wewe Baba 


Hakuna Kama Wewe Kathy Praise

Hakuna Kama Wewe

Now Playing...