Tumekuja Kukuchukua

By Bony Mwaitege

Lyrics

ieyee yaah hayaa yeeh

Tumekuja kukuchukua 

ieyee yaah hayaa yeeh

Tumekuja kukuchukua 


Bibi harusi (Tumekuja kukuchukua) 

Bibi harusi twende mama (Tumekuja kukuchukua) 

Bibi harusi (Tumekuja kukuchukua) 

Wazazi wako tumeelewana nao (Tumekuja kukuchukua) 

Wameturuhusu tuondoke nawe (Tumekuja kukuchukua) 


Tusingeweza kukuchukua bila ruhusa ya wazazi wako 

Ndio maana tulisafiri kwenda kuwaomba wazazi wako 

Ili turuhusiwe, zawadi mbali mbali tuliwapelekea 

Tunashukuru Mungu walizipokea 

Tulipowaomba tukuchukue 

Kuna taratibu tuliambiwa tuzifuate 

Taratibu zote tulizifwata,

Hapo ndipo tuliporuhusiwa 

Tumepewa baraka zote wewe uwe mke wa kijana wetu 

Bibi arusi wewe 

Tumepewa baraka zote wewe uingie kwenye ukoo wetu 

Bibi arusi wee


Tunamshukuru Jehovah (Tumekuja kukuchukua) 

Maombi yetu ameyasikia (Tumekuja kukuchukua) 

Tumeomba muda mrefu sana (Tumekuja kukuchukua) 

Kijana wetu apate mke (Tumekuja kukuchukua) 

Maombi yetu yamejibiwa (Tumekuja kukuchukua) 

Wewe ndiye jibu la maombi yetu (Tumekuja kukuchukua) 

Sisi unaotuona (Tumekuja kukuchukua) 

Ni ndugu wa Bwana arusi (Tumekuja kukuchukua) 

Tumesindikiza ndugu yetu (Tumekuja kukuchukua) 

Tumekuja kukuchukua wewe (Tumekuja kukuchukua) 

Tunawashukuru ndugu zako (Tumekuja kukuchukua) 

Wametupokea vizuri sana (Tumekuja kukuchukua) 

Bibi arusi twende wee (Tumekuja kukuchukua) 

Twende kwetu mama  


Tunatimiza maandiko (Tumekuja kukuchukua) 

Kama ilivyoandikwa (Tumekuja kukuchukua wewe) 

Mtu ataacha wazazi wake (Tumekuja kukuchukua) 

Ataambatana na mumewe (Tumekuja kukuchukua) 

Bibi arusi twende wee (Tumekuja kukuchukua) 

Malkia wetu twende (Tumekuja kukuchukua) 

Usiogope twende (Tumekuja kukuchukua) 

Yanatimizwa maandiko (Tumekuja kukuchukua)