Lyrics Page

Mwanangu

By Christina Shusho

2,017 views Jun 28, 2026 updated Verified editorial review

Christina Shusho's song 'Mwanangu' is a Swahili Christian song that serves as a parental warning to a child against yielding to the temptation of sinners. Drawing from Proverbs, it advises the child to avoid the paths of the wicked, whose words are sweet but whose end is bitter. The song emphasizes the fear of the Lord as the beginning of knowledge, urges obedience to parental teaching, and encourages holding fast to God's Word. It also calls for courage, gentleness, and respect for all people, regardless of status.

Lyrics Verified by Editorial Team

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Wakisema njoo nasi tuvizie ili kumwaga damu 

Tumwote asiye na haki, mwanangu usikubali 

Wana maneno matamu kama asali 

lakini mwisho mchungu kama shubiri 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Mwanangu usiende njiani pamoja nao 

Usienende katika mapito yao 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Miguu yao huenda mbio mauguni 

Na hufany haraka kumwaga damu 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Mwanangu kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa 

Bali wapumbavu hudharau hekima 

Mwanangu usikubali mwenye dhambi akushawishi 

Yasikilize sheria ya baba yako 

Na mafundisho ya mama yako 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Mwanangu mtego hutegwa bure 

Mbele ya macho ya ndege wowote 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Lishike sana neno la Mungu 

Uliandike kwenye kibao cha moyo 

Mwanangu usikubali mwenye dhambi akushawishi 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Uwe jasiri kama simba, mpole kama njiwa 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Ushike sana elimu, usimwache aende zake 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Heshimu wakubwa kwa wadogo,tajiri na fukara 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi  

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Mwanangu usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Usikubali wenye dhambi wakushawishi 

Music Video

Save Your Favorites

Create a free account to save songs, build your personal library, and connect with the Zion community.

Create Free Account

Join the Zion Community

Create a free account to save your favorite lyrics, submit song suggestions, and connect with fellow worshippers.

No spam. Unsubscribe anytime.