Neema

By Kambua

Lyrics

Ningekuwa jambo lakustahili sijui ningekuwa wapi 

Ningekuwa sababu ya matendo sijui ningetupwa wapi 

Ingekuwa kulingana na jina sijui ningeitwa nani 

Ningeitwa marehemu 

Ningeitwa mimi tasa

Ningeitwa aiyefaa 


Asante Yesu kwa neema yako 

Wokovu nimepata bure

Asante Yesu kwa neema yako 

Kukufa ningekufaa

Asante Yesu kwa neema yako 

Kutupwa ningetupwa 


Jalalani ungenipata nikila uchafu 

Msituni ungenikuta nikila majani 

(rudia)


Mnyonge mimi wangenidharau tu 

Dhaifu mimi wangenikanyaga tu

Sina nguvu mimi wangenimaliza tu 

Ningetupwa kwenye tanuru la moto niangamie 

Ningetupwa kwenye shimo la simba nifie huko 


Jalalani ungenipata nikila mchafu 

Msituni ungenikuta nikila majani 

(rudia)


Asante Yesu kwa neema yako 

Wokovu nimepata bure

Asante Yesu kwa neema yako 

Kukufa ningekufaa

Asante Yesu kwa neema yako 

Kutupwa ningetupwa 


Jalalani ungenipata nikila uchafu 

Msituni ungenikuta nikila majani 

(rudia)


Ni kwa neema (Neema)

Neema (neema)

Asante kwa neema (neeema)


Naishi kwa neema (Neema)

Neema (neema) neema (neema)

Naishi kwa neema (Neema)

Neema (neema) neema (neema)

Ni kwa neema yako 

Kambua - Neema (Official Music Video)