Umekuwa Nami

By Martha Mwangi

Lyrics

Baba nashukuru kwa yale yote umenitendea

Baba nashukuru kwa yale yote utatenda 

Umekuwa nami (Baba) Umekuwa nami (Baba) 

Nashukuru (Baba) Nashukuru (Baba) 


Kuna mengi nimeyaona nikadhani nimefika mwisho 

Mengi nimesikia yangenifanya nife moyo 

Lakini Baba ukatembea nami Hujaniacha 

Umekuwa nami (Baba) Umekuwa nami (Baba) 

Nashukuru (Baba) Nashukuru (Baba) 

Umekuwa nami Baba 


Machozi niliyolia Baba umeyapanguza 

Yote nilipoteza Baba umerejesha 

Imani yangu kwako Baba imerejeshwa 

Furaha iliyopotea nimeipata kwako 

Roho mtakatifu umenitia nguvu 

Roho mtakatifu umenitia nguvu 


Umekuwa nami (Baba) Umekuwa nami (Baba) 

Nashukuru (Baba) Nashukuru (Baba) 

Umekuwa nami Baba 


Umekuwa nami (Baba) Umekuwa nami (Baba) 

Nashukuru (Baba) Nashukuru (Baba) 

Umekuwa nami Baba