Mwaminifu

By Paul Clement

Lyrics

Una wasi wasi

Hofu na mashaka

Unahisi moyoni kama Mungu kakuacha

Maana unaona hausogei wala huendelei

Uko palepale kila siku

Uko vilevile (rudia 2)


Mungu aliianzisha safari tena ataimaliza

Maana alikujua kabla hujajijua kabla hujazaliwa  

Mungu hawezi kukuacha njiani

Safari yako aliianzisha mwenyewe

Asingetaka angekuacha mwanzoni

Unakokwenda yeye anajua 

(rudia 4)


Atainyosha njia yako 

Atainyosha njia yako 

Ina mabonde kweli

Ina vikwazo vingi

Atainyoosha njia yako

PAUL CLEMENT - MWAMINIFU