2 Wakorintho Mlango 1 2nd Corinthians

2 Wakorintho 1:1 2ndCorinthians 1:1

Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu; kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watakatifu wote walioko katika nchi yote ya Akaya.

2 Wakorintho 1:2 2ndCorinthians 1:2

Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

2 Wakorintho 1:3 2ndCorinthians 1:3

Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;

2 Wakorintho 1:4 2ndCorinthians 1:4

atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.

2 Wakorintho 1:5 2ndCorinthians 1:5

Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo.

2 Wakorintho 1:6 2ndCorinthians 1:6

Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi.

2 Wakorintho 1:7 2ndCorinthians 1:7

Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.

2 Wakorintho 1:8 2ndCorinthians 1:8

Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.

2 Wakorintho 1:9 2ndCorinthians 1:9

Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu,

2 Wakorintho 1:10 2ndCorinthians 1:10

aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa;

2 Wakorintho 1:11 2ndCorinthians 1:11

ninyi nanyi mkisaidiana nasi kwa ajili yetu katika kuomba, ili, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa msaada wa watu wengi, watu wengi watoe shukrani kwa ajili yetu.

2 Wakorintho 1:12 2ndCorinthians 1:12

Kwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa utakatifu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu; si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu; tulienenda katika dunia, na hasa kwenu ninyi.

2 Wakorintho 1:13 2ndCorinthians 1:13

Maana hatuwaandikii ninyi neno, ila yale msomayo, au kuyakiri; nami nataraji ya kuwa mtayakiri hayo hata mwisho;

2 Wakorintho 1:14 2ndCorinthians 1:14

vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana wetu Yesu.

2 Wakorintho 1:15 2ndCorinthians 1:15

Nami nikiwa na tumaini hilo nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili;

2 Wakorintho 1:16 2ndCorinthians 1:16

na kupita kwenu na kuendelea mpaka Makedonia; na tena toka Makedonia kurudi kwenu na kusafirishwa nanyi kwenda Uyahudi.

2 Wakorintho 1:17 2ndCorinthians 1:17

Basi, nilipokusudia hayo, je! Nalitumia kigeugeu? Au hayo niyakusudiayo, nayakusudia kwa jinsi ya mwili kwamba iwe hivi kwangu, kusema Ndiyo, ndiyo, na Siyo, siyo?

2 Wakorintho 1:18 2ndCorinthians 1:18

Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu si Ndiyo na siyo.

2 Wakorintho 1:19 2ndCorinthians 1:19

Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo.

2 Wakorintho 1:20 2ndCorinthians 1:20

Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.

2 Wakorintho 1:21 2ndCorinthians 1:21

Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,

2 Wakorintho 1:22 2ndCorinthians 1:22

naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.

2 Wakorintho 1:23 2ndCorinthians 1:23

Lakini mimi namwita Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijafika Korintho.

2 Wakorintho 1:24 2ndCorinthians 1:24

Si kwamba tunatawala imani yenu; bali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana kwa imani yenu mnasimama.