2 Wakorintho Mlango 4 2nd Corinthians

2 Wakorintho 4:1 2ndCorinthians 4:1

Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei;

2 Wakorintho 4:2 2ndCorinthians 4:2

lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.

2 Wakorintho 4:3 2ndCorinthians 4:3

Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;

2 Wakorintho 4:4 2ndCorinthians 4:4

ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

2 Wakorintho 4:5 2ndCorinthians 4:5

Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.

2 Wakorintho 4:6 2ndCorinthians 4:6

Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.

2 Wakorintho 4:7 2ndCorinthians 4:7

Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu.

2 Wakorintho 4:8 2ndCorinthians 4:8

Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa;

2 Wakorintho 4:9 2ndCorinthians 4:9

twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi;

2 Wakorintho 4:10 2ndCorinthians 4:10

siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu.

2 Wakorintho 4:11 2ndCorinthians 4:11

Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti.

2 Wakorintho 4:12 2ndCorinthians 4:12

Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu.

2 Wakorintho 4:13 2ndCorinthians 4:13

Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena;

2 Wakorintho 4:14 2ndCorinthians 4:14

tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi.

2 Wakorintho 4:15 2ndCorinthians 4:15

Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe.

2 Wakorintho 4:16 2ndCorinthians 4:16

Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.

2 Wakorintho 4:17 2ndCorinthians 4:17

Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;

2 Wakorintho 4:18 2ndCorinthians 4:18

tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.