2 Wakorintho Mlango 12 2nd Corinthians

2 Wakorintho 12:1 2ndCorinthians 12:1

Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana.

2 Wakorintho 12:2 2ndCorinthians 12:2

Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.

2 Wakorintho 12:3 2ndCorinthians 12:3

Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);

2 Wakorintho 12:4 2ndCorinthians 12:4

ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.

2 Wakorintho 12:5 2ndCorinthians 12:5

Kwa habari za mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika habari ya udhaifu wangu.

2 Wakorintho 12:6 2ndCorinthians 12:6

Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu.

2 Wakorintho 12:7 2ndCorinthians 12:7

Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.

2 Wakorintho 12:8 2ndCorinthians 12:8

Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.

2 Wakorintho 12:9 2ndCorinthians 12:9

Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

2 Wakorintho 12:10 2ndCorinthians 12:10

Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.

2 Wakorintho 12:11 2ndCorinthians 12:11

Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lo lote, nijapokuwa si kitu.

2 Wakorintho 12:12 2ndCorinthians 12:12

Kweli ishara za mtume zilitendwa katikati yenu katika saburi yote, kwa ishara na maajabu na miujiza.

2 Wakorintho 12:13 2ndCorinthians 12:13

Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, ila kwa kuwa mimi sikuwalemea? Mnisamehe udhalimu huu.

2 Wakorintho 12:14 2ndCorinthians 12:14

Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto.

2 Wakorintho 12:15 2ndCorinthians 12:15

Nami kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?

2 Wakorintho 12:16 2ndCorinthians 12:16

Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu naliwapata kwa hila.

2 Wakorintho 12:17 2ndCorinthians 12:17

Je! Mtu ye yote niliyemtuma kwenu, kwa mtu huyo naliwatoza kitu?

2 Wakorintho 12:18 2ndCorinthians 12:18

Nalimwonya Tito, nikamtuma ndugu yule pamoja naye. Je! Tito aliwatoza kitu? Je! Hatukuenenda kwa Roho yeye yule na katika nyayo zile zile?

2 Wakorintho 12:19 2ndCorinthians 12:19

Mwadhani hata sasa ya kuwa najidhuru kwenu! Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na hayo yote, wapenzi, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.

2 Wakorintho 12:20 2ndCorinthians 12:20

Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong'onezo, na majivuno, na ghasia;

2 Wakorintho 12:21 2ndCorinthians 12:21

nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya.