2 Wakorintho Mlango 8 2nd Corinthians

2 Wakorintho 8:1 2ndCorinthians 8:1

Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia;

2 Wakorintho 8:2 2ndCorinthians 8:2

maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao.

2 Wakorintho 8:3 2ndCorinthians 8:3

Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao;

2 Wakorintho 8:4 2ndCorinthians 8:4

wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii, na shirika hili la kuwahudumia watakatifu.

2 Wakorintho 8:5 2ndCorinthians 8:5

Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu.

2 Wakorintho 8:6 2ndCorinthians 8:6

Hata tukamwonya Tito kuwatimilizia neema hii kwenu kama vile yeye alivyotangulia kuianzisha.

2 Wakorintho 8:7 2ndCorinthians 8:7

Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia.

2 Wakorintho 8:8 2ndCorinthians 8:8

Sineni ili kuwaamuru, bali kwa bidii ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu.

2 Wakorintho 8:9 2ndCorinthians 8:9

Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.

2 Wakorintho 8:10 2ndCorinthians 8:10

Nami katika neno hili natoa shauri langu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, yapata mwaka, licha ya kutenda hata na kutaka pia.

2 Wakorintho 8:11 2ndCorinthians 8:11

Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.

2 Wakorintho 8:12 2ndCorinthians 8:12

Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.

2 Wakorintho 8:13 2ndCorinthians 8:13

Maana sisemi hayo, ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki;

2 Wakorintho 8:14 2ndCorinthians 8:14

bali mambo yawe sawasawa; wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa; ili mambo yawe sawasawa.

2 Wakorintho 8:15 2ndCorinthians 8:15

Kama ilivyoandikwa, Aliyekusanya vingi, hakuzidi, wala yeye aliyekusanya vichache hakupungukiwa.

2 Wakorintho 8:16 2ndCorinthians 8:16

Lakini ahimidiwe Mungu atiaye bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo wa Tito.

2 Wakorintho 8:17 2ndCorinthians 8:17

Maana aliyapokea kweli yale maonyo; tena, huku akizidi kuwa na bidii, alisafiri kwenda kwenu kwa hiari yake mwenyewe.

2 Wakorintho 8:18 2ndCorinthians 8:18

Na pamoja naye tukamtuma ndugu yule ambaye sifa zake katika Injili zimeenea makanisani mwote.

2 Wakorintho 8:19 2ndCorinthians 8:19

Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nasi katika jambo la neema hii, tunayoitumikia, ili Bwana atukuzwe, ukadhihirike utayari wetu.

2 Wakorintho 8:20 2ndCorinthians 8:20

Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia;

2 Wakorintho 8:21 2ndCorinthians 8:21

tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.

2 Wakorintho 8:22 2ndCorinthians 8:22

Nasi pamoja nao tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona mara nyingi katika mambo mengi kuwa ana bidii, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini kuu alilo nalo kwenu.

2 Wakorintho 8:23 2ndCorinthians 8:23

Basi mtu akitaka habari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami kwa ajili yenu; tena akitaka habari za ndugu zetu, wao ni mitume wa makanisa, na utukufu wa Kristo.

2 Wakorintho 8:24 2ndCorinthians 8:24

Basi waonyesheni mbele ya makanisa hakika ya upendo wenu, na ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu.