2 Wakorintho Mlango 6 2nd Corinthians

2 Wakorintho 6:1 2ndCorinthians 6:1

Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.

2 Wakorintho 6:2 2ndCorinthians 6:2

(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)

2 Wakorintho 6:3 2ndCorinthians 6:3

Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe;

2 Wakorintho 6:4 2ndCorinthians 6:4

bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;

2 Wakorintho 6:5 2ndCorinthians 6:5

katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga;

2 Wakorintho 6:6 2ndCorinthians 6:6

katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki;

2 Wakorintho 6:7 2ndCorinthians 6:7

katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;

2 Wakorintho 6:8 2ndCorinthians 6:8

kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli;

2 Wakorintho 6:9 2ndCorinthians 6:9

kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa;

2 Wakorintho 6:10 2ndCorinthians 6:10

kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.

2 Wakorintho 6:11 2ndCorinthians 6:11

Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa.

2 Wakorintho 6:12 2ndCorinthians 6:12

Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu.

2 Wakorintho 6:13 2ndCorinthians 6:13

Basi, ili mlipe kadiri ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), nanyi pia mkunjuliwe mioyo.

2 Wakorintho 6:14 2ndCorinthians 6:14

Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

2 Wakorintho 6:15 2ndCorinthians 6:15

Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

2 Wakorintho 6:16 2ndCorinthians 6:16

Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

2 Wakorintho 6:17 2ndCorinthians 6:17

Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.

2 Wakorintho 6:18 2ndCorinthians 6:18

Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,