2 Wakorintho Mlango 13 2nd Corinthians

2 Wakorintho 13:1 2ndCorinthians 13:1

Hii ndiyo mara ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.

2 Wakorintho 13:2 2ndCorinthians 13:2

Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia;

2 Wakorintho 13:3 2ndCorinthians 13:3

kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemaye ndani yangu, ambaye si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu.

2 Wakorintho 13:4 2ndCorinthians 13:4

Maana, alisulibiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; lakini tutaishi pamoja naye kwa uweza wa Mungu ulio kwenu.

2 Wakorintho 13:5 2ndCorinthians 13:5

Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa.

2 Wakorintho 13:6 2ndCorinthians 13:6

Lakini natumaini kama mtajua ya kuwa sisi hatukukataliwa.

2 Wakorintho 13:7 2ndCorinthians 13:7

Nasi twamwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, lakini ninyi mfanye lile lililo jema, tujapokuwa sisi tu kama waliokataliwa.

2 Wakorintho 13:8 2ndCorinthians 13:8

Maana hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli.

2 Wakorintho 13:9 2ndCorinthians 13:9

Maana twafurahi, iwapo sisi tu dhaifu, nanyi mmekuwa hodari. Tena twaomba hili nalo, kutimilika kwenu.

2 Wakorintho 13:10 2ndCorinthians 13:10

Kwa sababu hiyo, naandika haya nisipokuwapo, ili, nikiwapo, nisiutumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.

2 Wakorintho 13:11 2ndCorinthians 13:11

Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.

2 Wakorintho 13:12 2ndCorinthians 13:12

Salimianeni kwa busu takatifu.

2 Wakorintho 13:13 2ndCorinthians 13:13

Watakatifu wote wawasalimu.

2 Wakorintho 13:14 2ndCorinthians 13:14

Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.