2 Wakorintho Mlango 7 2nd Corinthians

2 Wakorintho 7:1 2ndCorinthians 7:1

Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.

2 Wakorintho 7:2 2ndCorinthians 7:2

Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu.

2 Wakorintho 7:3 2ndCorinthians 7:3

Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi mmo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja, na kuishi pamoja.

2 Wakorintho 7:4 2ndCorinthians 7:4

Ninao ujasiri mwingi kwenu; naona fahari kuu juu yenu. Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.

2 Wakorintho 7:5 2ndCorinthians 7:5

Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu.

2 Wakorintho 7:6 2ndCorinthians 7:6

Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito.

2 Wakorintho 7:7 2ndCorinthians 7:7

Wala si kwa kuja kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu habari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hata nikazidi kufurahi.

2 Wakorintho 7:8 2ndCorinthians 7:8

Kwa sababu, ijapokuwa naliwahuzunisha kwa waraka ule, sijuti; hata ikiwa nalijuta, naona ya kwamba waraka ule uliwahuzunisha, ingawa ni kwa kitambo tu.

2 Wakorintho 7:9 2ndCorinthians 7:9

Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote.

2 Wakorintho 7:10 2ndCorinthians 7:10

Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.

2 Wakorintho 7:11 2ndCorinthians 7:11

Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii kama nini ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionyesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.

2 Wakorintho 7:12 2ndCorinthians 7:12

Basi, ijapokuwa naliwaandikia, sikuandika kwa ajili yake yeye aliyedhulumu, wala si kwa ajili yake yeye aliyedhulumiwa, bali bidii yenu kwa ajili yetu ipate kudhihirishwa kwenu mbele za Mungu.

2 Wakorintho 7:13 2ndCorinthians 7:13

Kwa hiyo tulifarijiwa. Tena katika kufarijiwa kwetu tulifurahi sana kupita kiasi kwa sababu ya furaha ya Tito; maana roho yake imeburudishwa na ninyi nyote.

2 Wakorintho 7:14 2ndCorinthians 7:14

Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lo lote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.

2 Wakorintho 7:15 2ndCorinthians 7:15

Na mapenzi yake kwenu yamekuwa mengi kupita kiasi, akumbukapo kutii kwenu ninyi nyote, jinsi mlivyomkaribisha kwa hofu na kutetemeka.

2 Wakorintho 7:16 2ndCorinthians 7:16

Nafurahi, kwa sababu katika kila neno nina moyo mkuu kwa ajili yenu.