2 Wakorintho Mlango 11 2nd Corinthians

2 Wakorintho 11:1 2ndCorinthians 11:1

Laiti mngechukuliana nami katika upumbavu wangu kidogo! Naam, mchukuliane nami.

2 Wakorintho 11:2 2ndCorinthians 11:2

Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.

2 Wakorintho 11:3 2ndCorinthians 11:3

Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

2 Wakorintho 11:4 2ndCorinthians 11:4

Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!

2 Wakorintho 11:5 2ndCorinthians 11:5

Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa na kitu walicho nacho mitume walio wakuu.

2 Wakorintho 11:6 2ndCorinthians 11:6

Lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyejua kunena, hii si hali yangu katika elimu; ila katika kila neno tumedhihirishwa kwenu.

2 Wakorintho 11:7 2ndCorinthians 11:7

Je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira?

2 Wakorintho 11:8 2ndCorinthians 11:8

Naliwanyang'anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi.

2 Wakorintho 11:9 2ndCorinthians 11:9

Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda.

2 Wakorintho 11:10 2ndCorinthians 11:10

Kama vile ile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hakuna mtu atakayenifumba kinywa katika kujisifu huku, katika mipaka ya Akaya.

2 Wakorintho 11:11 2ndCorinthians 11:11

Kwa nini? Je! Ni kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua.

2 Wakorintho 11:12 2ndCorinthians 11:12

Lakini nifanyalo nitalifanya, ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi; ili kwamba katika neno hilo wajisifialo waonekane kuwa kama sisi.

2 Wakorintho 11:13 2ndCorinthians 11:13

Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.

2 Wakorintho 11:14 2ndCorinthians 11:14

Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

2 Wakorintho 11:15 2ndCorinthians 11:15

Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.

2 Wakorintho 11:16 2ndCorinthians 11:16

Nasema tena, mtu asidhani ya kuwa mimi ni mpumbavu; lakini mjaponidhania hivi, mnikubali kama mpumbavu; ili mimi nami nipate kujisifu ngaa kidogo.

2 Wakorintho 11:17 2ndCorinthians 11:17

Ninenalo silineni agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu.

2 Wakorintho 11:18 2ndCorinthians 11:18

Kwa sababu wengi wanajisifu kwa jinsi ya mwili, mimi nami nitajisifu.

2 Wakorintho 11:19 2ndCorinthians 11:19

Ninyi, kwa kuwa mna akili, mnachukuliana na wajinga kwa furaha.

2 Wakorintho 11:20 2ndCorinthians 11:20

Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni.

2 Wakorintho 11:21 2ndCorinthians 11:21

Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Walakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), mimi nami ninao ujasiri.

2 Wakorintho 11:22 2ndCorinthians 11:22

Wao ni Waebrania? Na mimi pia. Wao ni Waisraeli? Na mimi pia. Wao ni uzao wa Ibrahimu? Na mimi pia.

2 Wakorintho 11:23 2ndCorinthians 11:23

Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.

2 Wakorintho 11:24 2ndCorinthians 11:24

Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja.

2 Wakorintho 11:25 2ndCorinthians 11:25

Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;

2 Wakorintho 11:26 2ndCorinthians 11:26

katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang'anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;

2 Wakorintho 11:27 2ndCorinthians 11:27

katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.

2 Wakorintho 11:28 2ndCorinthians 11:28

Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote.

2 Wakorintho 11:29 2ndCorinthians 11:29

Ni nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu nami? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukiwe?

2 Wakorintho 11:30 2ndCorinthians 11:30

Ikinibidi kujisifu, nitajisifia mambo ya udhaifu wangu.

2 Wakorintho 11:31 2ndCorinthians 11:31

Mungu, Baba wa Bwana Yesu, aliye mtukufu hata milele, anajua ya kuwa sisemi uongo.

2 Wakorintho 11:32 2ndCorinthians 11:32

Huko Dameski liwali wa mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, ili kunikamata;

2 Wakorintho 11:33 2ndCorinthians 11:33

nami nikatelemshwa ndani ya kapu, katika dirisha la ukutani, nikaokoka katika mikono yake.