2 Wakorintho Mlango 2 2nd Corinthians

2 Wakorintho 2:1 2ndCorinthians 2:1

Lakini nafsini mwangu nalikusudia hivi, nisije kwenu tena kwa huzuni.

2 Wakorintho 2:2 2ndCorinthians 2:2

Maana mimi nikiwatia huzuni, basi ni nani anifurahishaye mimi ila yeye ahuzunishwaye nami?

2 Wakorintho 2:3 2ndCorinthians 2:3

Nami naliwaandikia neno lilo hilo, ili nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumaini ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia.

2 Wakorintho 2:4 2ndCorinthians 2:4

Maana katika dhiki nyingi na taabu ya moyo niliwaandikia na machozi mengi; si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu nilio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi.

2 Wakorintho 2:5 2ndCorinthians 2:5

Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi tu, bali kwa sehemu (nisije nikalemea mno), amewahuzunisha ninyi nyote.

2 Wakorintho 2:6 2ndCorinthians 2:6

Yamtosha mtu wa namna hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi;

2 Wakorintho 2:7 2ndCorinthians 2:7

hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi.

2 Wakorintho 2:8 2ndCorinthians 2:8

Kwa hiyo nawasihi kumthibitishia upendo wenu.

2 Wakorintho 2:9 2ndCorinthians 2:9

Maana naliandika kwa sababu hii pia, ili nipate bayana kwenu kwamba mmekuwa wenye kutii katika mambo yote.

2 Wakorintho 2:10 2ndCorinthians 2:10

Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo,

2 Wakorintho 2:11 2ndCorinthians 2:11

Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.

2 Wakorintho 2:12 2ndCorinthians 2:12

Basi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo, nikafunguliwa mlango katika Bwana,

2 Wakorintho 2:13 2ndCorinthians 2:13

sikuona raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia.

2 Wakorintho 2:14 2ndCorinthians 2:14

Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.

2 Wakorintho 2:15 2ndCorinthians 2:15

Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;

2 Wakorintho 2:16 2ndCorinthians 2:16

katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo?

2 Wakorintho 2:17 2ndCorinthians 2:17

Kwa maana sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.