2 Samweli Mlango 1 2nd Samuel

2 Samweli 1:1 2ndSamuel 1:1

Ikawa baada ya kufa kwake Sauli, hapo Daudi aliporudi katika kuwaua Waamaleki, naye Daudi amekaa siku mbili katika Siklagi;

2 Samweli 1:2 2ndSamuel 1:2

hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia.

2 Samweli 1:3 2ndSamuel 1:3

Daudi akamwambia, Umetoka wapi? Akamwambia, Nimeokoka katika kambi ya Israeli.

2 Samweli 1:4 2ndSamuel 1:4

Daudi akamwambia, Yalikwendaje? Tafadhali uniambie. Akajibu, Watu wamekimbia vitani, tena watu wengi wameanguka wamekufa; hata Sauli naye na Yonathani, mwanawe, wamekufa.

2 Samweli 1:5 2ndSamuel 1:5

Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Umejuaje ya kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?

2 Samweli 1:6 2ndSamuel 1:6

Yule kijana aliyempa habari akasema, Nalikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi.

2 Samweli 1:7 2ndSamuel 1:7

Naye alipotazama nyuma, akaniona, akaniita. Nikajibu, Mimi hapa.

2 Samweli 1:8 2ndSamuel 1:8

Akaniambia, U nani wewe? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki.

2 Samweli 1:9 2ndSamuel 1:9

Akaniambia, Tafadhali simama karibu nami, ukaniue, maana shida imenipata; kwa sababu roho yangu ingali hai ndani yangu.

2 Samweli 1:10 2ndSamuel 1:10

Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nalijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikaitwaa ile taji iliyokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.

2 Samweli 1:11 2ndSamuel 1:11

Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye;

2 Samweli 1:12 2ndSamuel 1:12

wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa Bwana na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.

2 Samweli 1:13 2ndSamuel 1:13

Naye Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Watoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.

2 Samweli 1:14 2ndSamuel 1:14

Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi wa BWANA?

2 Samweli 1:15 2ndSamuel 1:15

Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa.

2 Samweli 1:16 2ndSamuel 1:16

Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa Bwana.

2 Samweli 1:17 2ndSamuel 1:17

Basi Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya;

2 Samweli 1:18 2ndSamuel 1:18

(kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari), akasema, Wana wa Yuda na wafundishwe haya,

2 Samweli 1:19 2ndSamuel 1:19

Walio fahari yako, Ee Israeli Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa; Jinsi mashujaa walivyoanguka!

2 Samweli 1:20 2ndSamuel 1:20

Msiyahubiri mambo haya katika Gathi, Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni; Wasije wakashangilia binti za Wafilisti, Binti za wasiotahiriwa wakasimanga.

2 Samweli 1:21 2ndSamuel 1:21

Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenu Umande wala mvua, wala mashamba ya matoleo; Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa, Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta.

2 Samweli 1:22 2ndSamuel 1:22

Kutoka kwa damu yao waliouawa, Kutoka kwa shahamu yao mashujaa, Upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, Wala upanga wa Sauli haukurudi bure.

2 Samweli 1:23 2ndSamuel 1:23

Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.

2 Samweli 1:24 2ndSamuel 1:24

Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu.

2 Samweli 1:25 2ndSamuel 1:25

Jinsi mashujaa walivyoanguka Katikati ya vita! Ee Yonathani, wewe umeuawa Juu ya mahali pako palipoinuka

2 Samweli 1:26 2ndSamuel 1:26

Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana; Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, Kupita upendo wa wanawake.

2 Samweli 1:27 2ndSamuel 1:27

Jinsi mashujaa walivyoanguka, Na silaha za vita zilivyoangamia!