2 Samweli Mlango 22 2nd Samuel

2 Samweli 22:1 2ndSamuel 22:1

Basi Daudi akamwambia Bwana maneno ya wimbo huu, siku ile Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake zote, na mkononi mwa Sauli;

2 Samweli 22:2 2ndSamuel 22:2

akasema, Bwana ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu, naam, wangu;

2 Samweli 22:3 2ndSamuel 22:3

Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri.

2 Samweli 22:4 2ndSamuel 22:4

Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa; Hivyo nitaokoka na adui zangu.

2 Samweli 22:5 2ndSamuel 22:5

Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.

2 Samweli 22:6 2ndSamuel 22:6

Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili.

2 Samweli 22:7 2ndSamuel 22:7

Katika shida yangu nalimwita Bwana, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu;

2 Samweli 22:8 2ndSamuel 22:8

Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasuka-suka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.

2 Samweli 22:9 2ndSamuel 22:9

Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala; Makaa yakawashwa nao.

2 Samweli 22:10 2ndSamuel 22:10

Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.

2 Samweli 22:11 2ndSamuel 22:11

Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo.

2 Samweli 22:12 2ndSamuel 22:12

Akafanya giza hema zake za kumzunguka, Makusanyiko ya maji, mawingu makuu ya mbinguni.

2 Samweli 22:13 2ndSamuel 22:13

Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Makaa ya moto yakawashwa.

2 Samweli 22:14 2ndSamuel 22:14

Bwana alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye juu akaitoa sauti yake.

2 Samweli 22:15 2ndSamuel 22:15

Akapiga mishale, akawatawanya; Umeme, naye akawatapanya.

2 Samweli 22:16 2ndSamuel 22:16

Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake Bwana, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.

2 Samweli 22:17 2ndSamuel 22:17

Alipeleka kutoka juu, akanishika; Akanitoa katika maji mengi;

2 Samweli 22:18 2ndSamuel 22:18

Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia; Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.

2 Samweli 22:19 2ndSamuel 22:19

Walinikabili siku ya msiba wangu; Lakini Bwana alikuwa tegemeo langu.

2 Samweli 22:20 2ndSamuel 22:20

Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.

2 Samweli 22:21 2ndSamuel 22:21

Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.

2 Samweli 22:22 2ndSamuel 22:22

Maana nimezishika njia za Bwana, Wala sikumwasi Mungu wangu.

2 Samweli 22:23 2ndSamuel 22:23

Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu; Na kwa habari za amri zake, sikuziacha.

2 Samweli 22:24 2ndSamuel 22:24

Nami nalikuwa mkamilifu kwake, Nikajilinda na uovu wangu.

2 Samweli 22:25 2ndSamuel 22:25

Basi Bwana amenilipa sawasawa na haki yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.

2 Samweli 22:26 2ndSamuel 22:26

Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;

2 Samweli 22:27 2ndSamuel 22:27

Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi.

2 Samweli 22:28 2ndSamuel 22:28

Na watu wanaoonewa wewe utawaokoa; Ila macho yako ni juu ya wenye kiburi, uwadhili.

2 Samweli 22:29 2ndSamuel 22:29

Kwa kuwa wewe u taa yangu, Ee Bwana; Na Bwana ataniangazia giza langu.

2 Samweli 22:30 2ndSamuel 22:30

Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi; Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta.

2 Samweli 22:31 2ndSamuel 22:31

Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya Bwana imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia.

2 Samweli 22:32 2ndSamuel 22:32

Maana ni nani aliye Mungu, ila Bwana? Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu?

2 Samweli 22:33 2ndSamuel 22:33

Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu; Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake.

2 Samweli 22:34 2ndSamuel 22:34

Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.

2 Samweli 22:35 2ndSamuel 22:35

Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba.

2 Samweli 22:36 2ndSamuel 22:36

Nawe umenipa ngao ya wokovu wako; Na unyenyekevu wako umenikuza.

2 Samweli 22:37 2ndSamuel 22:37

Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Wala miguu yangu haikuteleza.

2 Samweli 22:38 2ndSamuel 22:38

Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza; Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa.

2 Samweli 22:39 2ndSamuel 22:39

Nami nimewakomesha na kuwapiga-piga wasiweze kusimama; Naam, wameanguka chini ya miguu yangu.

2 Samweli 22:40 2ndSamuel 22:40

Maana umenifunga mshipi wa nguvu kwa vita; Umenitiishia chini yangu walioniondokea.

2 Samweli 22:41 2ndSamuel 22:41

Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo, Ili niwakatilie mbali wanaonichukia.

2 Samweli 22:42 2ndSamuel 22:42

Walitazama, lakini hakuna wa kuokoa; Walimwita Bwana, lakini hakuwajibu.

2 Samweli 22:43 2ndSamuel 22:43

Ndipo nikawaponda kama mavumbi ya nchi, Nikawakanyaga kama matope ya njiani, nikawatawanya.

2 Samweli 22:44 2ndSamuel 22:44

Nawe umeniokoa na mashindano ya watu wangu; Umenihifadhi niwe kichwa cha mataifa; Watu nisiowajua watanitumikia.

2 Samweli 22:45 2ndSamuel 22:45

Wageni watanijia wakinyenyekea; Kwa kusikia tu habari zangu, Mara watanitii.

2 Samweli 22:46 2ndSamuel 22:46

Wageni nao watatepetea, Watatoka katika ngome zao wakitetemeka.

2 Samweli 22:47 2ndSamuel 22:47

Bwana ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa mwamba wa wokovu wangu;

2 Samweli 22:48 2ndSamuel 22:48

Naam, Mungu anipatiaye kisasi, Na kuwatweza watu chini yangu,

2 Samweli 22:49 2ndSamuel 22:49

Na kunileta nje nitoke kwa adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia; Waniponya na mtu wa jeuri.

2 Samweli 22:50 2ndSamuel 22:50

Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.

2 Samweli 22:51 2ndSamuel 22:51

Ampa mfalme wake wokovu mkuu; Amfanyia fadhili masihi wake Daudi na mzao wake ,hata milele.