2 Samweli Mlango 23 2nd Samuel

2 Samweli 23:1 2ndSamuel 23:1

Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi. Daudi, mwana wa Yese, anena, anena huyo mtu aliyeinuliwa juu, Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo,Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;

2 Samweli 23:2 2ndSamuel 23:2

Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu.

2 Samweli 23:3 2ndSamuel 23:3

Mungu wa Israeli alisema, Mwamba wa Israeli aliniambia, Atawalaye wanadamu kwa haki, Akitawala katika kicho cha Mungu,

2 Samweli 23:4 2ndSamuel 23:4

Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo, Asubuhi isiyo na mawingu.

2 Samweli 23:5 2ndSamuel 23:5

Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za Bwana? Kwa kuwa amefanya nami agano la milele; Ina taratibu katika yote, ni thabiti, Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.

2 Samweli 23:6 2ndSamuel 23:6

Lakini hatawachipuza watu wa ubatili; Watakuwa wote kama miiba ya nyikani ya kutupwa, Ambayo haivuniki kwa mkono,

2 Samweli 23:7 2ndSamuel 23:7

Mtu atakayeigusa hiyo, Na awe na chuma na mpini wa mkuki, Nao watateketezwa papo hapo kwa moto.

2 Samweli 23:8 2ndSamuel 23:8

Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu Mhakmoni,mkuu wa maakida ;huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja.

2 Samweli 23:9 2ndSamuel 23:9

Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao;

2 Samweli 23:10 2ndSamuel 23:10

huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye Bwana akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu.

2 Samweli 23:11 2ndSamuel 23:11

Na baada yake kulikuwa na Shama, mwana wa Agee, Mharari; nao Wafilisti walikuwa wamekusanyika huko Lehi, palipokuwapo konde lililojaa midengu; nao watu wakawakimbia Wafilisti;

2 Samweli 23:12 2ndSamuel 23:12

ila huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye Bwana akafanya wokovu mkuu.

2 Samweli 23:13 2ndSamuel 23:13

Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.

2 Samweli 23:14 2ndSamuel 23:14

Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu.

2 Samweli 23:15 2ndSamuel 23:15

Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango!

2 Samweli 23:16 2ndSamuel 23:16

Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana.

2 Samweli 23:17 2ndSamuel 23:17

Akasema, Hasha, Bwana, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.

2 Samweli 23:18 2ndSamuel 23:18

Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu.

2 Samweli 23:19 2ndSamuel 23:19

Je! Huyo hakuwa na heshima maalumu miongoni mwa wale watatu? Kwa hiyo akawekwa kuwa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu.

2 Samweli 23:20 2ndSamuel 23:20

Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wakali wawili wa Moabu, pia akashuka akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theruji.

2 Samweli 23:21 2ndSamuel 23:21

huyo naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe.

2 Samweli 23:22 2ndSamuel 23:22

Hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu.

2 Samweli 23:23 2ndSamuel 23:23

Alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake.

2 Samweli 23:24 2ndSamuel 23:24

Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmojawapo wa wale thelathini; na Elhanani, mwana wa Dodo, wa Bethlehemu;

2 Samweli 23:25 2ndSamuel 23:25

na Shama, Mharodi, na Elika, Mharodi;

2 Samweli 23:26 2ndSamuel 23:26

na Helesi, Mpeloni, na Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi;

2 Samweli 23:27 2ndSamuel 23:27

na Abiezeri, Mwanathothi, na Sibekai, Mhushathi;

2 Samweli 23:28 2ndSamuel 23:28

na Salmoni, Mwahohi, na Maharai, Mnetofathi;

2 Samweli 23:29 2ndSamuel 23:29

na Heledi, mwana wa Baana, Mnetofathi, na Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini;

2 Samweli 23:30 2ndSamuel 23:30

na Benaya, Mpirathoni, na Hurai, wa vijito vya Gaashi;

2 Samweli 23:31 2ndSamuel 23:31

na Abieli, Mwarbathi, na Azmawethi, Mbarhumi;

2 Samweli 23:32 2ndSamuel 23:32

na Eliaba, Mshaalboni, na wana wa Yasheni; na Yonathani,

2 Samweli 23:33 2ndSamuel 23:33

mwana wa Shama, Mharari, na Ahiamu, mwana wa Shalali, Mharari;

2 Samweli 23:34 2ndSamuel 23:34

na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;

2 Samweli 23:35 2ndSamuel 23:35

na Hezro, Mkarmeli, na Paarai, Mwarbi;

2 Samweli 23:36 2ndSamuel 23:36

na Igali, mwana wa Nathani, wa Soba, na Bani, Mgadi;

2 Samweli 23:37 2ndSamuel 23:37

na Seleki, Mwamoni, na Naharai, Mbeerothi, ambao ni wachukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya;

2 Samweli 23:38 2ndSamuel 23:38

na Ira, Mwithri, na Garebu, Mwithri;

2 Samweli 23:39 2ndSamuel 23:39

na Uria, Mhiti; jumla yao ilikuwa watu thelathini na saba.