2 Samweli Mlango 10 2nd Samuel

2 Samweli 10:1 2ndSamuel 10:1

Ikawa baadaye, mfalme wa wana wa Amori akafa, akamiliki Hanuni, mwanawe, mahali pake.

2 Samweli 10:2 2ndSamuel 10:2

Naye Daudi akasema, Nitamtendea wema Hanuni, mwana wa Nahasi, kama babaye alivyonitendea wema mimi. Basi Daudi akatuma kwa mkono wa watumishi wake, ili kumtuliza kwa habari za babaye. Wakaja watumishi wa Daudi katika nchi ya wana wa Amoni.

2 Samweli 10:3 2ndSamuel 10:3

Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, bwana wao, Je! Waona ya kuwa Daudi amemheshimu babayo kwa kutuma kwako wafariji? Je! Daudi hakuwapeleka watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, na kuupeleleza, na kuuangamiza?

2 Samweli 10:4 2ndSamuel 10:4

Basi Hanuni akawatwaa hao watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao, akawakatia nguo zao katikati, hata matakoni, akawatoa waende zao.

2 Samweli 10:5 2ndSamuel 10:5

Watu walipomwambia Daudi habari hizo, akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wametahayarika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi.

2 Samweli 10:6 2ndSamuel 10:6

Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, wana wa Amoni wakatuma na kuwaajiri Washami wa Bethrehobu, na Washami wa Soba, askari ishirini elfu, na mfalme wa Maaka mwenye watu elfu, na watu wa Tobu watu kumi na mbili elfu.

2 Samweli 10:7 2ndSamuel 10:7

Naye Daudi aliposikia akamtuma Yoabu, na jeshi lote la mashujaa.

2 Samweli 10:8 2ndSamuel 10:8

Wana wa Amoni wakatoka, wakapanga vita mahali pa kuingilia lango; na Washami wa Soba, na wa Rehobu, na watu wa Tobu, na wa Maaka, walikuwa peke yao uwandani.

2 Samweli 10:9 2ndSamuel 10:9

Basi Yoabu alipoona ya kwamba uso wa vita umekuwa juu yake mbele na nyuma, akachagua baadhi ya wateule wote wa Israeli, akawapanga juu ya Washami;

2 Samweli 10:10 2ndSamuel 10:10

akawatia nguvu watu waliosalia mkononi mwa Abishai, nduguye, akawapanga juu ya wana wa Amoni.

2 Samweli 10:11 2ndSamuel 10:11

Akasema, Wakiwa Washami hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia, lakini wana wa Amoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakuja nikusaidie wewe.

2 Samweli 10:12 2ndSamuel 10:12

Uwe hodari, tukajitie moyo mkuu, kwa ajili ya watu wetu, na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu; naye Bwana afanye yaliyo mema machoni pake.

2 Samweli 10:13 2ndSamuel 10:13

Basi Yoabu na watu waliokuwa pamoja naye wakakaribia kupigana na Washami; nao wakakimbia mbele yake.

2 Samweli 10:14 2ndSamuel 10:14

Na wana wa Amoni walipoona ya kwamba Washami wamekimbia, wakakimbia nao mbele ya Abishai, wakaingia mjini. Ndipo Yoabu akarudi kutoka kwa wana wa Amoni, akaja Yerusalemu.

2 Samweli 10:15 2ndSamuel 10:15

Na Washami walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, wakakusanyika.

2 Samweli 10:16 2ndSamuel 10:16

Naye Hadadezeri akatuma na kuwaleta Washami waliokuwako ng'ambo ya Mto; nao wakaja Helamu, naye Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza.

2 Samweli 10:17 2ndSamuel 10:17

Alipoambiwa Daudi, akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akaja Helamu. Nao Washami wakajipanga kinyume cha Daudi, wakapigana naye.

2 Samweli 10:18 2ndSamuel 10:18

Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi arobaini elfu, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko.

2 Samweli 10:19 2ndSamuel 10:19

Na wafalme wote waliomtumikia Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Israeli, wakawatumikia. Basi Washami wakaogopa kuwasaidia wana wa Amoni tena.