Matendo ya Mitume Mlango 28 Acts

Matendo ya Mitume 28:1 Acts 28:1

Tulipokwisha kuokoka, ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita.

Matendo ya Mitume 28:2 Acts 28:2

Wenyeji wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana waliwasha moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyonyesha na kwa sababu ya baridi.

Matendo ya Mitume 28:3 Acts 28:3

Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzonga-zonga mkononi.

Matendo ya Mitume 28:4 Acts 28:4

Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewa-lewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi.

Matendo ya Mitume 28:5 Acts 28:5

Lakini yeye akamtukusia motoni asipate madhara.

Matendo ya Mitume 28:6 Acts 28:6

Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu.

Matendo ya Mitume 28:7 Acts 28:7

Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya mkuu wa kisiwa, jina lake Publio; mtu huyu akatukaribisha kwa moyo wa urafiki, akatufanya wageni wake kwa muda wa siku tatu.

Matendo ya Mitume 28:8 Acts 28:8

Ikawa babaake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paulo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, na kumpoza.

Matendo ya Mitume 28:9 Acts 28:9

Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja wakapozwa;

Matendo ya Mitume 28:10 Acts 28:10

nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi; basi tulipoabiri wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo.

Matendo ya Mitume 28:11 Acts 28:11

Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha.

Matendo ya Mitume 28:12 Acts 28:12

Tukafika Sirakusa, tukakaa siku tatu.

Matendo ya Mitume 28:13 Acts 28:13

Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio; baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli.

Matendo ya Mitume 28:14 Acts 28:14

Huko tukakuta ndugu, wakatusihi tukae nao siku saba; na hivi tukafika Rumi.

Matendo ya Mitume 28:15 Acts 28:15

Na kutoka huko ndugu, waliposikia habari zetu, wakaja kutulaki mpaka Soko la Apio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona alimshukuru Mungu, akachangamka.

Matendo ya Mitume 28:16 Acts 28:16

Tulipoingia Rumi Paulo alipewa ruhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda.

Matendo ya Mitume 28:17 Acts 28:17

Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane, hata walipokutanika akawaambia, Ndugu zangu, ningawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, hali nimefungwa, tokea Yerusalemu.

Matendo ya Mitume 28:18 Acts 28:18

Na hao walipokwisha kuniuliza-uliza walitaka kunifungua, kwa maana hapakuwa na sababu yo yote kwangu ya kuuawa.

Matendo ya Mitume 28:19 Acts 28:19

Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu.

Matendo ya Mitume 28:20 Acts 28:20

Basi kwa ajili ya hayo, nimewaita mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli.

Matendo ya Mitume 28:21 Acts 28:21

Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye habari zako kutoka Uyahudi, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa na kutupasha habari, au kunena neno baya juu yako.

Matendo ya Mitume 28:22 Acts 28:22

Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika habari za madhehebu hiyo imejulikana kwetu kwamba inanenwa vibaya kila mahali.

Matendo ya Mitume 28:23 Acts 28:23

Wakiisha kuagana naye siku, wakamjia katika nyumba aliyokaa, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii, tangu asubuhi hata jioni.

Matendo ya Mitume 28:24 Acts 28:24

Wengine waliamini yale yaliyonenwa, wengine hawakuyaamini.

Matendo ya Mitume 28:25 Acts 28:25

Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,

Matendo ya Mitume 28:26 Acts 28:26

akisema, Enenda kwa watu hawa, ukawaambie, Kusikia, mtasikia wala hamtafahamu; Na kuona, mtaona wala hamtatambua;

Matendo ya Mitume 28:27 Acts 28:27

Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni mazito ya kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya.

Matendo ya Mitume 28:28 Acts 28:28

Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa, nao watasikia!

Matendo ya Mitume 28:29 Acts 28:29

Alipokwisha kusema hayo, Wayahudi wakaenda zao, wakiulizana mengi wao kwa wao.]

Matendo ya Mitume 28:30 Acts 28:30

Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea,

Matendo ya Mitume 28:31 Acts 28:31

akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu.