Matendo ya Mitume Mlango 9 Acts

Matendo ya Mitume 9:1 Acts 9:1

Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,

Matendo ya Mitume 9:2 Acts 9:2

akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.

Matendo ya Mitume 9:3 Acts 9:3

Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.

Matendo ya Mitume 9:4 Acts 9:4

Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?

Matendo ya Mitume 9:5 Acts 9:5

Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.

Matendo ya Mitume 9:6 Acts 9:6

Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.

Matendo ya Mitume 9:7 Acts 9:7

Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu.

Matendo ya Mitume 9:8 Acts 9:8

Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.

Matendo ya Mitume 9:9 Acts 9:9

Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.

Matendo ya Mitume 9:10 Acts 9:10

Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.

Matendo ya Mitume 9:11 Acts 9:11

Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;

Matendo ya Mitume 9:12 Acts 9:12

naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.

Matendo ya Mitume 9:13 Acts 9:13

Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu;

Matendo ya Mitume 9:14 Acts 9:14

hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako.

Matendo ya Mitume 9:15 Acts 9:15

Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.

Matendo ya Mitume 9:16 Acts 9:16

Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.

Matendo ya Mitume 9:17 Acts 9:17

Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.

Matendo ya Mitume 9:18 Acts 9:18

Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;

Matendo ya Mitume 9:19 Acts 9:19

akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.

Matendo ya Mitume 9:20 Acts 9:20

Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.

Matendo ya Mitume 9:21 Acts 9:21

Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewaharibu walioliitia Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuwa amekuja kwa kusudi hilo, awafunge na kuwapeleka kwa wakuu wa makuhani?

Matendo ya Mitume 9:22 Acts 9:22

Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.

Matendo ya Mitume 9:23 Acts 9:23

Hata siku nyingi zilipopita, Wayahudi wakafanya shauri ili wamwue;

Matendo ya Mitume 9:24 Acts 9:24

lakini hila yao ikajulikana na Sauli. Wakamvizia malangoni mchana na usiku wapate kumwua.

Matendo ya Mitume 9:25 Acts 9:25

Wanafunzi wake wakamtwaa usiku wakamshusha ukutani, wakimtelemsha katika kapu.

Matendo ya Mitume 9:26 Acts 9:26

Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi.

Matendo ya Mitume 9:27 Acts 9:27

Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu.

Matendo ya Mitume 9:28 Acts 9:28

Naye akawa pamoja nao katika Yerusalemu akiingia na kutoka.

Matendo ya Mitume 9:29 Acts 9:29

Akahubiri kwa jina la Bwana kwa ushujaa, akinena na kuhojiana na Wayahudi wa Kiyunani. Nao wakajaribu kumwua.

Matendo ya Mitume 9:30 Acts 9:30

Lakini ndugu walipopata habari wakamchukua mpaka Kaisaria, wakampeleka aende Tarso.

Matendo ya Mitume 9:31 Acts 9:31

Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.

Matendo ya Mitume 9:32 Acts 9:32

Hata Petro alipokuwa akizunguka-zunguka pande zote akawatelemkia na watakatifu waliokaa Lida.

Matendo ya Mitume 9:33 Acts 9:33

Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza.

Matendo ya Mitume 9:34 Acts 9:34

Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka.

Matendo ya Mitume 9:35 Acts 9:35

Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona, wakamgeukia Bwana.

Matendo ya Mitume 9:36 Acts 9:36

Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.

Matendo ya Mitume 9:37 Acts 9:37

Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.

Matendo ya Mitume 9:38 Acts 9:38

Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu.

Matendo ya Mitume 9:39 Acts 9:39

Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.

Matendo ya Mitume 9:40 Acts 9:40

Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.

Matendo ya Mitume 9:41 Acts 9:41

Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai.

Matendo ya Mitume 9:42 Acts 9:42

Ikajulikana katika mji mzima wa Yafa; watu wengi wakamwamini Bwana.

Matendo ya Mitume 9:43 Acts 9:43

Basi Petro akakaa siku kadha wa kadha huko Yafa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi.