Mambo ya Walawi Mlango 1 Leviticus

Mambo ya Walawi 1:1 Leviticus 1:1

Bwana akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia,

Mambo ya Walawi 1:2 Leviticus 1:2

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea Bwana matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng'ombe na katika kondoo.

Mambo ya Walawi 1:3 Leviticus 1:3

Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe mume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya Bwana.

Mambo ya Walawi 1:4 Leviticus 1:4

Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.

Mambo ya Walawi 1:5 Leviticus 1:5

Naye atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Bwana; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kando-kando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania

Mambo ya Walawi 1:6 Leviticus 1:6

Kisha atachuna sadaka ya kuteketeza na kuikata vipande vyake.

Mambo ya Walawi 1:7 Leviticus 1:7

Kisha wana wa Haruni, watatia moto juu ya madhabahu, na kuzipanga kuni juu ya moto,

Mambo ya Walawi 1:8 Leviticus 1:8

kisha wana wa Haruni, makuhani, watazipanga kuni zilizo juu ya moto uliopo juu ya madhabahu;

Mambo ya Walawi 1:9 Leviticus 1:9

lakini matumbo yake, na miguu yake, ataiosha kwa maji; na huyo kuhani ataviteketeza vyote juu ya madhabahu, ili iwe sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.

Mambo ya Walawi 1:10 Leviticus 1:10

Na matoleo yake kwamba ni katika kundi, katika kondoo, au katika mbuzi, kuwa sadaka ya kuteketezwa; atatoa mume mkamilifu.

Mambo ya Walawi 1:11 Leviticus 1:11

Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za Bwana; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote.

Mambo ya Walawi 1:12 Leviticus 1:12

Kisha atamkata vipande vyake, pamoja na kichwa chake, na mafuta yake; kisha atavipanga vile vipande juu ya kuni zilizo juu ya madhabahu;

Mambo ya Walawi 1:13 Leviticus 1:13

lakini matumbo yake, na miguu yake, ataosha kwa maji; na huyo kuhani atavisongeza vyote na kuviteketeza juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.

Mambo ya Walawi 1:14 Leviticus 1:14

Na matoleo yake atakayomtolea Bwana kuwa sadaka ya kuteketezwa, kwamba ni katika ndege, ndipo atakapoleta matoleo yake katika hua au katika makinda ya njiwa.

Mambo ya Walawi 1:15 Leviticus 1:15

Kisha kuhani atamleta karibu na madhabahu, naye atamkongonyoa kichwa, na kumteketeza kwa moto juu ya madhabahu; na damu yake itachuruzishwa kando ya madhabahu;

Mambo ya Walawi 1:16 Leviticus 1:16

kisha atakiondoa kile kibofu chake, pamoja na taka zake, na kukitupa kando ya madhabahu upande wa mashariki, mahali pa majivu;

Mambo ya Walawi 1:17 Leviticus 1:17

kisha atampasua na mabawa yake, lakini asimkate vipande viwili; kisha kuhani atamteketeza juu ya madhabahu, juu ya kuni zilizo juu ya moto; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.