Mambo ya Walawi Mlango 26 Leviticus

Mambo ya Walawi 26:1 Leviticus 26:1

Msifanye sanamu yo yote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Mambo ya Walawi 26:2 Leviticus 26:2

Zishikeni Sabato zangu, na kupastahi patakatifu pangu; mimi ndimi Bwana.

Mambo ya Walawi 26:3 Leviticus 26:3

Kama mkienda katika amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyafanya;

Mambo ya Walawi 26:4 Leviticus 26:4

ndipo nitazinyesha mvua zenu kwa nyakati zake, na nchi itazaa maongeo yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake.

Mambo ya Walawi 26:5 Leviticus 26:5

Tena kupura nafaka kwenu kutaendelea hata wakati wa kuvuna zabibu, na kuvuna zabibu kutaendelea hata wakati wa kupanda mbegu; nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, na kuketi katika nchi yenu salama.

Mambo ya Walawi 26:6 Leviticus 26:6

Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala wala hapana atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu.

Mambo ya Walawi 26:7 Leviticus 26:7

Nanyi mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele zenu kwa upanga.

Mambo ya Walawi 26:8 Leviticus 26:8

Na watu watano wa kwenu watawafukuza watu mia, na watu mia wa kwenu watawafukuza watu elfu kumi; na adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga.

Mambo ya Walawi 26:9 Leviticus 26:9

Nami nitawaelekezea uso wangu, na kuwapa uzazi mwingi, na kuwaongeza; nami nitalithibitisha agano langu pamoja nanyi.

Mambo ya Walawi 26:10 Leviticus 26:10

Nanyi mtakula akiba ya zamani mliyoiweka siku nyingi, tena hayo ya zamani mtayatoa, ili myaweke yaliyo mapya.

Mambo ya Walawi 26:11 Leviticus 26:11

Nami nitaiweka maskani yangu kati yenu; wala roho yangu haitawachukia.

Mambo ya Walawi 26:12 Leviticus 26:12

Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.

Mambo ya Walawi 26:13 Leviticus 26:13

Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawaendesha mwende sawasawa.

Mambo ya Walawi 26:14 Leviticus 26:14

Lakini msiponisikiza, wala hamtaki kuyafanya maagizo hayo yote;

Mambo ya Walawi 26:15 Leviticus 26:15

nanyi mkizikataa amri zangu, na roho yenu ikichukia hukumu zangu, hata ikawa hamtaki kuyafanya maagizo yangu yote, bali mwalivunja agano langu;

Mambo ya Walawi 26:16 Leviticus 26:16

mimi nami nitawatenda jambo hili; nitaamrisha uje juu yenu utisho, hata kifua kikuu na homa, zitakazoharibu macho yenu, na kuidhoofisha roho; nanyi mtapanda mbegu yenu bure, kwa kuwa adui zenu wataila.

Mambo ya Walawi 26:17 Leviticus 26:17

Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye.

Mambo ya Walawi 26:18 Leviticus 26:18

Tena ikiwa baada ya hayo hamtaki kunisikiza, ndipo nitawaadhibu zaidi mara saba kwa ajili ya dhambi zenu.

Mambo ya Walawi 26:19 Leviticus 26:19

Nami nitakivunja kiburi cha uwezo wenu; nami nitazifanya mbingu zenu kuwa kama chuma, na nchi yenu kuwa kama shaba;

Mambo ya Walawi 26:20 Leviticus 26:20

na nguvu zenu mtazitumia bure; kwa kuwa nchi yenu haitazaa mazao yake, wala miti ya nchi haitazaa matunda yake.

Mambo ya Walawi 26:21 Leviticus 26:21

Nanyi ikiwa mwaenenda kinyume changu, wala hamtaki kunisikiza; nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, kama dhambi zenu zilivyo.

Mambo ya Walawi 26:22 Leviticus 26:22

Nami nitaleta wanyama wakali kati yenu, ambao watawanyang'anya watoto wenu, na kuwaharibu wanyama wenu wa kufugwa, na kuwapunguza muwe wachache hesabu yenu; na njia zenu zitakuwa ni ukiwa.

Mambo ya Walawi 26:23 Leviticus 26:23

Tena kama hamtaki kurejezwa upya kwangu mimi kwa mambo haya, bali mwaendelea kunishikia kinyume; ndipo mimi nami nitaendelea kuwashikia ninyi kinyume;

Mambo ya Walawi 26:24 Leviticus 26:24

nami nitawapiga, naam mimi, mara saba kwa ajili ya dhambi zenu.

Mambo ya Walawi 26:25 Leviticus 26:25

Nami nitaleta upanga juu yenu, utakaopatiliza kisasi cha hilo agano; nanyi mtakutanishwa ndani ya miji yenu; nami nitaleta tauni kati yenu; nanyi mtatiwa mkononi mwa adui.

Mambo ya Walawi 26:26 Leviticus 26:26

Hapo nitakapovunja tegemeo lenu la mkate, wanawake kumi wataoka mikate yenu katika tanuu moja, nao watawapa mikate yenu tena kwa kupima kwa mizani; nanyi mtakula, lakini hamtashiba.

Mambo ya Walawi 26:27 Leviticus 26:27

Tena ikiwa baada ya hayo yote hamtaki kunisikiza, bali mwaenenda kwa kunishikia kinyume;

Mambo ya Walawi 26:28 Leviticus 26:28

ndipo nami nitakwenda kwa kuwashikia ninyi kinyume katika ghadhabu yangu; nami nitawaadhibu mara saba kwa dhambi zenu.

Mambo ya Walawi 26:29 Leviticus 26:29

Nanyi mtakula nyama ya miili ya wana wenu, na nyama ya miili ya binti zenu mtaila.

Mambo ya Walawi 26:30 Leviticus 26:30

Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia.

Mambo ya Walawi 26:31 Leviticus 26:31

Nami nitaifanya miji yenu iwe maganjo, na mahali penu patakatifu nitapatia ukiwa; wala sitasikia harufu ya manukato yenu yapendezayo.

Mambo ya Walawi 26:32 Leviticus 26:32

Nami nitaitia hiyo nchi ukiwa; na adui zenu watakaokaa huko wataistaajabia.

Mambo ya Walawi 26:33 Leviticus 26:33

Nanyi nitawatapanya-tapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ni ukiwa, na miji yenu maganjo.

Mambo ya Walawi 26:34 Leviticus 26:34

Hapo ndipo nchi itakapozifurahia Sabato zake, wakati itakapokuwa hali ya ukiwa, nanyi mtakapokuwa katika nchi ya adui zenu; ndipo nchi itakapopumzika, na kuzifurahia Sabato zake.

Mambo ya Walawi 26:35 Leviticus 26:35

Wakati wote itakapokuwa na ukiwa, itapumzika; ni hayo mapumziko ambayo haikuwa nayo katika Sabato zenu, hapo mlipokaa katika nchi hiyo.

Mambo ya Walawi 26:36 Leviticus 26:36

Tena hao wa kwenu watakaobaki, nitawatilia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye.

Mambo ya Walawi 26:37 Leviticus 26:37

Nao wataangukiana wenyewe kwa wenyewe, kama mbele ya upanga, hapo ambapo hapana afukuzaye; wala hamtakuwa na nguvu za kusimama mbele ya adui zenu.

Mambo ya Walawi 26:38 Leviticus 26:38

Nanyi mtaangamia kati ya mataifa, na nchi ya adui zenu itawameza.

Mambo ya Walawi 26:39 Leviticus 26:39

Na watu wa kwenu watakaobaki watafifia kwa ajili ya uovu wao, katika hizo nchi za adui zenu; tena watafifia kwa ajili ya uovu wa baba zao, pamoja nao.

Mambo ya Walawi 26:40 Leviticus 26:40

Nao wataukiri uovu wao, na uovu wa baba zao, katika maasi yao waliyoasi juu yangu, tena ya kuwa kwa sababu wameendelea kunishikia kinyume,

Mambo ya Walawi 26:41 Leviticus 26:41

mimi nami nimeendelea kuwashikia kinyume wao, na kuwatia katika nchi ya adui zao; lakini hapo, kama mioyo yao isiyokuwa tohara ikinyenyekea, nao wakubali adhabu ya uovu wao;

Mambo ya Walawi 26:42 Leviticus 26:42

ndipo nitakapokumbuka agano langu pamoja na Yakobo, tena agano langu na Isaka, tena agano langu na Ibrahimu nitalikumbuka; nami nitaikumbuka nchi hiyo.

Mambo ya Walawi 26:43 Leviticus 26:43

Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu, naam, ni kwa sababu wamezikataa hukumu zangu, na roho zao zimezichukia amri zangu.

Mambo ya Walawi 26:44 Leviticus 26:44

Lakini pamoja na hayo yote, watakapokuwa katika nchi ya adui zao, mimi, sitawatupa, wala sitawachukia, niwaangamize kabisa, na kulivunja agano langu pamoja nao; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao;

Mambo ya Walawi 26:45 Leviticus 26:45

lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano la baba zao, niliowaleta watoke katika nchi ya Misri mbele ya macho ya mataifa, ili kwamba niwe Mungu wao; mimi ndimi Bwana.

Mambo ya Walawi 26:46 Leviticus 26:46

Hizi ni amri na hukumu na sheria, Bwana alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.