Mambo ya Walawi Mlango 24 Leviticus

Mambo ya Walawi 24:1 Leviticus 24:1

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

Mambo ya Walawi 24:2 Leviticus 24:2

Waagize wana wa Israeli kwamba wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya ile nuru, ili hiyo taa iwake daima.

Mambo ya Walawi 24:3 Leviticus 24:3

Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza tangu jioni hata asubuhi mbele za Bwana daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu.

Mambo ya Walawi 24:4 Leviticus 24:4

Atazitengeza hizo taa katika kile kinara kilicho safi mbele za Bwana daima.

Mambo ya Walawi 24:5 Leviticus 24:5

Nawe utatwaa unga mwembamba, na kuoka mikate kumi na miwili ya huo unga; sehemu za kumi mbili za efa, zitakuwa katika mkate mmoja.

Mambo ya Walawi 24:6 Leviticus 24:6

Nawe iweke mistari miwili, mikate sita kwa kila mstari, juu ya hiyo meza safi, mbele za Bwana.

Mambo ya Walawi 24:7 Leviticus 24:7

Nawe utatia ubani safi juu ya kila mstari, ili uwe ukumbusho kwa hiyo mikate, sadaka ya kusongezwa kwa Bwana kwa moto.

Mambo ya Walawi 24:8 Leviticus 24:8

Kila siku ya Sabato ataipanga mbele za Bwana daima; ni kwa ajili ya wana wa Israeli, agano la milele.

Mambo ya Walawi 24:9 Leviticus 24:9

Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zisongezwazo kwa Bwana kwa moto, kwa amri ya milele.

Mambo ya Walawi 24:10 Leviticus 24:10

Ikawa mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, ambaye babaye alikuwa Mmisri, akatokea kati ya wana wa Israeli; na huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, na Mwisraeli mmoja, wakapigana pamoja ndani ya marago;

Mambo ya Walawi 24:11 Leviticus 24:11

kisha huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru hilo Jina, na kuapiza; nao wakamleta kwa Musa. Na jina la mamaye alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila ya Dani.

Mambo ya Walawi 24:12 Leviticus 24:12

Nao wakamtia kifungoni, ili wapate kuambiwa neno litakalotoka kinywani pa Bwana.

Mambo ya Walawi 24:13 Leviticus 24:13

Na Bwana akasema na Musa, na kumwambia,

Mambo ya Walawi 24:14 Leviticus 24:14

Mtoe huyo aliyeapiza nje ya marago; na wale wote waliomsikia na waweke mikono yao kichwani mwake, kisha mkutano wote na wamwue kwa kumpiga kwa mawe.

Mambo ya Walawi 24:15 Leviticus 24:15

Nawe nena na wana wa Israeli na kuwaambia, Mtu awaye yote atakayemlaani Mungu wake atachukua dhambi yake.

Mambo ya Walawi 24:16 Leviticus 24:16

Na yeye atakayelikufuru jina la Bwana hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la Bwana atauawa.

Mambo ya Walawi 24:17 Leviticus 24:17

Na mtu ampigaye mtu hata akafa, lazima atauawa;

Mambo ya Walawi 24:18 Leviticus 24:18

na atakayempiga mnyama hata akafa atalipa; uhai kwa uhai.

Mambo ya Walawi 24:19 Leviticus 24:19

Na mtu akimtia mwenziwe kilema; vile vile kama alivyofanya, naye atafanyiwa vivyo;

Mambo ya Walawi 24:20 Leviticus 24:20

jeraha kwa jeraha, jicho kwa jicho, jino kwa jino; vile vile kama alivyomtia mtu kilema, naye atalipwa vivyo.

Mambo ya Walawi 24:21 Leviticus 24:21

Na mtu amwuaye mnyama atalipa; na yeye atakayemwua binadamu atauawa.

Mambo ya Walawi 24:22 Leviticus 24:22

Mtakuwa na sheria moja tu, kwa huyo aliye mgeni, na kwa mzalia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Mambo ya Walawi 24:23 Leviticus 24:23

Musa akanena na wana wa Israeli, nao wakamtoa huyo aliyeapiza nje ya marago, wakamwua kwa kumpiga kwa mawe. Wana wa Israeli wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Musa.