Mambo ya Walawi Mlango 9 Leviticus

Mambo ya Walawi 9:1 Leviticus 9:1

Basi ilikuwa siku ya nane, Musa akawaita Haruni na wanawe, pamoja na wazee wa Israeli;

Mambo ya Walawi 9:2 Leviticus 9:2

akamwambia Haruni, Twaa wewe mwana-ng'ombe mume awe sadaka ya dhambi, na kondoo mume wa sadaka ya kuteketezwa, wakamilifu, ukawasongeze mbele ya Bwana.

Mambo ya Walawi 9:3 Leviticus 9:3

Nawe utawaambia wana wa Israeli, ukisema, Twaeni mbuzi mume awe sadaka ya dhambi; na mwana-ng'ombe, na mwana-kondoo, wote wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, kwa sadaka ya kuteketezwa;

Mambo ya Walawi 9:4 Leviticus 9:4

na ng'ombe mume, na kondoo mume, kwa sadaka za amani, ili kuwachinja mbele za Bwana; na sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta; kwa maana, Bwana hivi leo atawatokea.

Mambo ya Walawi 9:5 Leviticus 9:5

Nao wakayaleta hayo yaliyoagizwa na Musa wakayaweka mbele ya hema ya kukutania; kisha mkutano wote ukakaribia wakasimama mbele za Bwana.

Mambo ya Walawi 9:6 Leviticus 9:6

Kisha Musa akasema, Neno aliloliagiza Bwana kwamba mlifanye ni hili; na huo utukufu wa Bwana utawatokea.

Mambo ya Walawi 9:7 Leviticus 9:7

Musa akamwambia Haruni, Ikaribie madhabahu, uitoe sadaka yako ya dhambi, na sadaka yako ya kuteketezwa, ukafanye upatanisho kwa ajili ya nafsi yako, na kwa ajili ya watu; nawe uitoe hiyo dhabihu ya watu, ukafanye upatanisho kwa ajili yao; kama Bwana alivyoagiza.

Mambo ya Walawi 9:8 Leviticus 9:8

Basi Haruni akakaribia madhabahuni, akamchinja huyo mwana-ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliyekuwa kwa ajili ya nafsi yake.

Mambo ya Walawi 9:9 Leviticus 9:9

Kisha wana wa Haruni wakamsongezea Haruni ile damu; naye akatia kidole chake katika damu, na kuitia katika pembe za madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu;

Mambo ya Walawi 9:10 Leviticus 9:10

lakini mafuta, na figo, na kitambi kilichotoka katika ini ya hiyo sadaka ya dhambi, akaviteketeza juu ya madhabahu, kama Bwana alivyomwagiza Musa.

Mambo ya Walawi 9:11 Leviticus 9:11

Na nyama, na ngozi akazichoma moto nje ya marago.

Mambo ya Walawi 9:12 Leviticus 9:12

Naye akaichinja sadaka ya kuteketezwa; na wanawe Haruni wakamsongezea ile damu, naye akainyunyiza katika madhabahu pande zote.

Mambo ya Walawi 9:13 Leviticus 9:13

Nao wakamletea sadaka ya kuteketezwa kipande kwa kipande, na kichwa; naye akaviteketeza juu ya madhabahu.

Mambo ya Walawi 9:14 Leviticus 9:14

Kisha akaosha matumbo, na miguu na kuiteketeza juu ya hiyo sadaka ya kuteketezwa madhabahuni.

Mambo ya Walawi 9:15 Leviticus 9:15

Kisha akaisongeza dhabihu ya watu, akamtwaa mbuzi wa sadaka ya dhambi aliyekuwa kwa hao watu, na kumchinja, na kumtoa kwa ajili ya dhambi kama yule wa kwanza.

Mambo ya Walawi 9:16 Leviticus 9:16

Kisha akaisongeza sadaka ya kuteketezwa, na kuitoa sawasawa na sheria.

Mambo ya Walawi 9:17 Leviticus 9:17

Kisha akaisongeza sadaka ya unga, na kutwaa konzi humo, na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi.

Mambo ya Walawi 9:18 Leviticus 9:18

Huyo ng'ombe mume naye akamchinja, na huyo kondoo mume pia, dhabihu ya sadaka za amani, zilizokuwa kwa ajili ya watu; na wanawe Haruni wakamsongezea ile damu, naye akainyunyiza katika madhabahu pande zote,

Mambo ya Walawi 9:19 Leviticus 9:19

na mafuta ya ng'ombe; na ya kondoo, mkia wake wa mafuta, na hayo yafunikayo matumbo, na figo zake, na kitambi cha ini;

Mambo ya Walawi 9:20 Leviticus 9:20

nao wakayaweka hayo mafuta juu ya vidari, naye akayateketeza mafuta juu ya madhabahu;

Mambo ya Walawi 9:21 Leviticus 9:21

na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kuume, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele ya Bwana; kama Musa alivyoagiza.

Mambo ya Walawi 9:22 Leviticus 9:22

Kisha Haruni akainua mikono yake na kuielekeza kwa hao watu, akawabariki; kisha akashuka akisha isongeza sadaka ya dhambi, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani.

Mambo ya Walawi 9:23 Leviticus 9:23

Kisha Musa na Haruni wakaingia ndani ya hema ya kukutania, kisha wakatoka nje, na kuwabarikia watu; na huo utukufu wa Bwana ukawatokea watu wote.

Mambo ya Walawi 9:24 Leviticus 9:24

Kisha moto ukatoka hapo mbele za Bwana, na kuiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na yale mafuta juu ya madhabahu; watu wote walipouona huo moto wakapiga kelele wakainama kifudifudi.