Mambo ya Walawi Mlango 18 Leviticus

Mambo ya Walawi 18:1 Leviticus 18:1

Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

Mambo ya Walawi 18:2 Leviticus 18:2

Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Mambo ya Walawi 18:3 Leviticus 18:3

Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mliyokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msiende katika amri zao hao.

Mambo ya Walawi 18:4 Leviticus 18:4

Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Mambo ya Walawi 18:5 Leviticus 18:5

Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi Bwana.

Mambo ya Walawi 18:6 Leviticus 18:6

Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana.

Mambo ya Walawi 18:7 Leviticus 18:7

Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.

Mambo ya Walawi 18:8 Leviticus 18:8

Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako.

Mambo ya Walawi 18:9 Leviticus 18:9

Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue.

Mambo ya Walawi 18:10 Leviticus 18:10

Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe.

Mambo ya Walawi 18:11 Leviticus 18:11

Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake.

Mambo ya Walawi 18:12 Leviticus 18:12

Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu.

Mambo ya Walawi 18:13 Leviticus 18:13

Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu.

Mambo ya Walawi 18:14 Leviticus 18:14

Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako.

Mambo ya Walawi 18:15 Leviticus 18:15

Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo.

Mambo ya Walawi 18:16 Leviticus 18:16

Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.

Mambo ya Walawi 18:17 Leviticus 18:17

Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu.

Mambo ya Walawi 18:18 Leviticus 18:18

Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai.

Mambo ya Walawi 18:19 Leviticus 18:19

Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake.

Mambo ya Walawi 18:20 Leviticus 18:20

Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.

Mambo ya Walawi 18:21 Leviticus 18:21

Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana.

Mambo ya Walawi 18:22 Leviticus 18:22

Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.

Mambo ya Walawi 18:23 Leviticus 18:23

Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko.

Mambo ya Walawi 18:24 Leviticus 18:24

Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote;

Mambo ya Walawi 18:25 Leviticus 18:25

na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa.

Mambo ya Walawi 18:26 Leviticus 18:26

Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu;

Mambo ya Walawi 18:27 Leviticus 18:27

(kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)

Mambo ya Walawi 18:28 Leviticus 18:28

ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu.

Mambo ya Walawi 18:29 Leviticus 18:29

Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao.

Mambo ya Walawi 18:30 Leviticus 18:30

Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.