Mambo ya Walawi Mlango 3 Leviticus

Mambo ya Walawi 3:1 Leviticus 3:1

Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng'ombe, mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya Bwana.

Mambo ya Walawi 3:2 Leviticus 3:2

Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.

Mambo ya Walawi 3:3 Leviticus 3:3

Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo,

Mambo ya Walawi 3:4 Leviticus 3:4

na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno, na hicho kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa.

Mambo ya Walawi 3:5 Leviticus 3:5

Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana.

Mambo ya Walawi 3:6 Leviticus 3:6

Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia Bwana, kwamba ni katika kundi la kondoo; mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu.

Mambo ya Walawi 3:7 Leviticus 3:7

Kama akimtoa mwana-kondoo kuwa matoleo yake, ndipo atakapomtolea Bwana;

Mambo ya Walawi 3:8 Leviticus 3:8

naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemsongeza, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.

Mambo ya Walawi 3:9 Leviticus 3:9

Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani dhabihu kwa Bwana, itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yake, na mkia wenye mafuta mzima, atauondoa kwa kuukata hapo karibu na mfupa wa maungoni; na mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo,

Mambo ya Walawi 3:10 Leviticus 3:10

na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa.

Mambo ya Walawi 3:11 Leviticus 3:11

Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto.

Mambo ya Walawi 3:12 Leviticus 3:12

Na matoleo yake, kwamba ni mbuzi, ndipo atakapomtoa mbele za Bwana;

Mambo ya Walawi 3:13 Leviticus 3:13

naye ataweka mkono wake kichwani mwake, na kumchinja hapo mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.

Mambo ya Walawi 3:14 Leviticus 3:14

Naye atasongeza katika sadaka hiyo matoleo yake, dhabihu kwa Bwana kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo,

Mambo ya Walawi 3:15 Leviticus 3:15

na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini pamoja na hizo figo mbili; hayo yote atayaondoa.

Mambo ya Walawi 3:16 Leviticus 3:16

Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya Bwana.

Mambo ya Walawi 3:17 Leviticus 3:17

Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.