Warumi Mlango 16 Romans

Warumi 16:1 Romans 16:1

Namkabidhi kwenu Fibi, ndugu yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea;

Warumi 16:2 Romans 16:2

kwamba mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia.

Warumi 16:3 Romans 16:3

Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu;

Warumi 16:4 Romans 16:4

waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia; nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao.

Warumi 16:5 Romans 16:5

Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo.

Warumi 16:6 Romans 16:6

Nisalimieni Mariamu, aliyejitaabisha sana kwa ajili yenu.

Warumi 16:7 Romans 16:7

Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.

Warumi 16:8 Romans 16:8

Nisalimieni Ampliato, mpenzi wangu katika Bwana.

Warumi 16:9 Romans 16:9

Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi, mpenzi wangu.

Warumi 16:10 Romans 16:10

Nisalimieni Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Aristobulo.

Warumi 16:11 Romans 16:11

Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Narkiso, walio katika Bwana.

Warumi 16:12 Romans 16:12

Nisalimieni Trifaina na Trifosa, wenye bidii katika Bwana. Nisalimieni Persisi, mpenzi aliyejitahidi sana katika Bwana.

Warumi 16:13 Romans 16:13

Nisalimieni Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliye mama yangu pia.

Warumi 16:14 Romans 16:14

Nisalimieni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma, na ndugu walio pamoja nao.

Warumi 16:15 Romans 16:15

Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na watakatifu wote walio pamoja nao.

Warumi 16:16 Romans 16:16

Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu.

Warumi 16:17 Romans 16:17

Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.

Warumi 16:18 Romans 16:18

Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu.

Warumi 16:19 Romans 16:19

Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.

Warumi 16:20 Romans 16:20

Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]

Warumi 16:21 Romans 16:21

Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yasoni, na Sosipatro, jamaa zangu.

Warumi 16:22 Romans 16:22

Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana.

Warumi 16:23 Romans 16:23

Gayo, mwenyeji wangu na wa Kanisa lote pia awasalimu. Erasto, wakili wa mji, awasalimu, na Kwarto, ndugu yetu.

Warumi 16:24 Romans 16:24

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.]

Warumi 16:25 Romans 16:25

Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele,

Warumi 16:26 Romans 16:26

ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani.

Warumi 16:27 Romans 16:27

Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina.