Warumi Mlango 12 Romans

Warumi 12:1 Romans 12:1

Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

Warumi 12:2 Romans 12:2

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Warumi 12:3 Romans 12:3

Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.

Warumi 12:4 Romans 12:4

Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;

Warumi 12:5 Romans 12:5

Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.

Warumi 12:6 Romans 12:6

Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;

Warumi 12:7 Romans 12:7

ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;

Warumi 12:8 Romans 12:8

mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.

Warumi 12:9 Romans 12:9

Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.

Warumi 12:10 Romans 12:10

Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;

Warumi 12:11 Romans 12:11

kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;

Warumi 12:12 Romans 12:12

kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;

Warumi 12:13 Romans 12:13

kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.

Warumi 12:14 Romans 12:14

Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.

Warumi 12:15 Romans 12:15

Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.

Warumi 12:16 Romans 12:16

Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.

Warumi 12:17 Romans 12:17

Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.

Warumi 12:18 Romans 12:18

Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.

Warumi 12:19 Romans 12:19

Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.

Warumi 12:20 Romans 12:20

Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.

Warumi 12:21 Romans 12:21

Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.