Warumi Mlango 4 Romans

Warumi 4:1 Romans 4:1

Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili?

Warumi 4:2 Romans 4:2

Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu.

Warumi 4:3 Romans 4:3

Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.

Warumi 4:4 Romans 4:4

Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.

Warumi 4:5 Romans 4:5

Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.

Warumi 4:6 Romans 4:6

Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,

Warumi 4:7 Romans 4:7

Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao.

Warumi 4:8 Romans 4:8

Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi.

Warumi 4:9 Romans 4:9

Basi je! Uheri huo ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba kwake Ibrahimu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki.

Warumi 4:10 Romans 4:10

Alihesabiwaje basi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa.

Warumi 4:11 Romans 4:11

Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki;

Warumi 4:12 Romans 4:12

tena awe baba ya kutahiriwa, kwa wale ambao si waliotahiriwa tu, bali pia wanazifuata nyayo za imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa.

Warumi 4:13 Romans 4:13

Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa imani.

Warumi 4:14 Romans 4:14

Maana ikiwa wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika.

Warumi 4:15 Romans 4:15

Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.

Warumi 4:16 Romans 4:16

Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote;

Warumi 4:17 Romans 4:17

(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.

Warumi 4:18 Romans 4:18

Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.

Warumi 4:19 Romans 4:19

Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.

Warumi 4:20 Romans 4:20

Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;

Warumi 4:21 Romans 4:21

huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.

Warumi 4:22 Romans 4:22

Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.

Warumi 4:23 Romans 4:23

Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake;

Warumi 4:24 Romans 4:24

bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;

Warumi 4:25 Romans 4:25

ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.