Warumi Mlango 14 Romans

Warumi 14:1 Romans 14:1

Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake.

Warumi 14:2 Romans 14:2

Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.

Warumi 14:3 Romans 14:3

Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali.

Warumi 14:4 Romans 14:4

Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.

Warumi 14:5 Romans 14:5

Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.

Warumi 14:6 Romans 14:6

Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.

Warumi 14:7 Romans 14:7

Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake.

Warumi 14:8 Romans 14:8

Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.

Warumi 14:9 Romans 14:9

Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.

Warumi 14:10 Romans 14:10

Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.

Warumi 14:11 Romans 14:11

Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.

Warumi 14:12 Romans 14:12

Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Warumi 14:13 Romans 14:13

Basi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali toeni hukumu hii, mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha.

Warumi 14:14 Romans 14:14

Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.

Warumi 14:15 Romans 14:15

Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.

Warumi 14:16 Romans 14:16

Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.

Warumi 14:17 Romans 14:17

Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.

Warumi 14:18 Romans 14:18

Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.

Warumi 14:19 Romans 14:19

Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.

Warumi 14:20 Romans 14:20

Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza.

Warumi 14:21 Romans 14:21

Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.

Warumi 14:22 Romans 14:22

Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.

Warumi 14:23 Romans 14:23

Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.