Warumi Mlango 3 Romans

Warumi 3:1 Romans 3:1

Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini?

Warumi 3:2 Romans 3:2

Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.

Warumi 3:3 Romans 3:3

Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?

Warumi 3:4 Romans 3:4

Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.

Warumi 3:5 Romans 3:5

Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.)

Warumi 3:6 Romans 3:6

Hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu?

Warumi 3:7 Romans 3:7

Lakini, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi?

Warumi 3:8 Romans 3:8

Kwa nini tusiseme (kama tulivyosingiziwa, na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo), Na tufanye mabaya, ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki.

Warumi 3:9 Romans 3:9

Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi;

Warumi 3:10 Romans 3:10

kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.

Warumi 3:11 Romans 3:11

Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.

Warumi 3:12 Romans 3:12

Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.

Warumi 3:13 Romans 3:13

Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao.

Warumi 3:14 Romans 3:14

Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.

Warumi 3:15 Romans 3:15

Miguu yao ina mbio kumwaga damu.

Warumi 3:16 Romans 3:16

Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao.

Warumi 3:17 Romans 3:17

Wala njia ya amani hawakuijua.

Warumi 3:18 Romans 3:18

Kumcha Mungu hakupo machoni pao.

Warumi 3:19 Romans 3:19

Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;

Warumi 3:20 Romans 3:20

kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.

Warumi 3:21 Romans 3:21

Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii;

Warumi 3:22 Romans 3:22

ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;

Warumi 3:23 Romans 3:23

kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

Warumi 3:24 Romans 3:24

wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;

Warumi 3:25 Romans 3:25

ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa.

Warumi 3:26 Romans 3:26

apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu.

Warumi 3:27 Romans 3:27

Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani.

Warumi 3:28 Romans 3:28

Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.

Warumi 3:29 Romans 3:29

Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia;

Warumi 3:30 Romans 3:30

kama kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo.

Warumi 3:31 Romans 3:31

Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.