Warumi Mlango 15 Romans

Warumi 15:1 Romans 15:1

Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.

Warumi 15:2 Romans 15:2

Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe.

Warumi 15:3 Romans 15:3

Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi.

Warumi 15:4 Romans 15:4

Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.

Warumi 15:5 Romans 15:5

Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu;

Warumi 15:6 Romans 15:6

ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Warumi 15:7 Romans 15:7

Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe.

Warumi 15:8 Romans 15:8

Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;

Warumi 15:9 Romans 15:9

tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.

Warumi 15:10 Romans 15:10

Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na watu wake.

Warumi 15:11 Romans 15:11

Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana; Enyi watu wote,mhimidini.

Warumi 15:12 Romans 15:12

Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini.

Warumi 15:13 Romans 15:13

Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Warumi 15:14 Romans 15:14

Ndugu zangu, nimehakikishwa mimi mwenyewe kwa habari zenu ya kuwa ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana.

Warumi 15:15 Romans 15:15

Lakini nawaandikia, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba kuwakumbusha, kwa neema ile niliyopewa na Mungu,

Warumi 15:16 Romans 15:16

ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.

Warumi 15:17 Romans 15:17

Basi, nina sababu ya kuona fahari katika Kristo Yesu mbele za Mungu.

Warumi 15:18 Romans 15:18

Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo,

Warumi 15:19 Romans 15:19

kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kando kando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu;

Warumi 15:20 Romans 15:20

kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine;

Warumi 15:21 Romans 15:21

bali kama ilivyoandikwa, Wale wasiohubiriwa habari zake wataona, Na wale wasiojasikia watafahamu.

Warumi 15:22 Romans 15:22

Ndiyo sababu nalizuiwa mara nyingi nisije kwenu.

Warumi 15:23 Romans 15:23

Lakini sasa, kwa kuwa sina wasaa tena pande hizi, tena tangu miaka mingi nina shauku kuja kwenu;

Warumi 15:24 Romans 15:24

wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Spania [nitakuja kwenu.] Kwa maana nataraji kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kusafirishwa nanyi, moyo wangu ushibe kwenu kidogo.

Warumi 15:25 Romans 15:25

Ila sasa ninakwenda Yerusalemu, nikiwahudumu watakatifu;

Warumi 15:26 Romans 15:26

maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu huko Yerusalemu walio maskini.

Warumi 15:27 Romans 15:27

Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumu kwa mambo yao ya mwili.

Warumi 15:28 Romans 15:28

Basi nikiisha kuimaliza kazi hiyo, na kuwatilia muhuri tunda hilo, nitapitia kwenu, kwenda Spania.

Warumi 15:29 Romans 15:29

Nami najua ya kuwa nikija kwenu nitakuja kwa utimilifu wa baraka ya Kristo.

Warumi 15:30 Romans 15:30

Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu;

Warumi 15:31 Romans 15:31

kwamba niokolewe na wale wasioamini katika Uyahudi, na tena huduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemu ikubalike kwa watakatifu;

Warumi 15:32 Romans 15:32

nipate kufika kwenu kwa furaha, kama apendavyo Mungu, nikapate kupumzika pamoja nanyi.

Warumi 15:33 Romans 15:33

Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina.