Nikumbushe

By Bahati

Lyrics

Usiponiona leo kama jana kesho nikumbushe

Nisipokuwa leo kama jana kesho unikumbushe 

Usiponiona leo kama jana kesho nikumbushe

Nisipokuwa leo kama jana kesho unikumbushe

Nikumbushe eh unikumbushe eh

Leo nyota imeng'aa nasahau nilikotoka

Naidharau mitaa na mateso niliyosota, aie

Ndugu zangu kinyaa mafukara wananichosha

Niache wafe na njaa nijisifu nitawanyosha eh

Sili kwetu Kisumu bondo, chakula haina swaga,

Sitaki kula chapo dondo nataka pizza na buger ehh,

Uniepushe maulana nisiishie njiani,

Unikumbushe ya jana, kesho nipe dhamani

Kwenye maisha ya muziki, ukiwa na uendo utaishi

Timu hazijengi urafiki, tusije kuuana kwa kugombania viti

Eti nimuache mama kwenye dhiki, kisa mambo yangu yametiki

Akipiga simu siishiki, nikipokea nimwone kama shabiki

Usiponiona leo kama jana kesho nikumbushe

Nisipokuwa leo kama jana kesho unikumbushe 

Usiponiona leo kama jana kesho nikumbushe

Nisipokuwa leo kama jana kesho unikumbushe

Nikumbushe eh unikumbushe eh

Nimejawa na kiburi, ukweli haupo nami,

Alionifunzage dini mama, simwiti mummy,

Roho imejawa na uhuni, star najiona mi

Nikipita na kagari vumbi , natupia wadhee

niwe kama peter, kumkana yesu mara tatu nikumbushe

Niwe kama jonah, kukataa kutumwa nineveh nikumbushe

Ah mwanabujah alionipa suporti, namtusi ilimradi iwe kiki

Walionipa jina mashabiki leo, nawaona wanafiki

Usiponiona leo kama jana kesho nikumbushe

Nisipokuwa leo kama jana kesho unikumbushe 

Usiponiona leo kama jana kesho nikumbushe

Nisipokuwa leo kama jana kesho unikumbushe

Nikumbushe eh unikumbushe eh

Bahati ft Rayvanny - Nikumbushe ( Official Music Video )