Lyrics Page

Wewe ni Mungu

By Sarah Magesa

2,172 views Jun 25, 2026 updated Verified editorial review

Sarah Magesa's song 'Wewe Ni Mungu' is a Swahili Christian worship song that declares God's sovereignty and protection over the believer. The lyrics affirm that God has chosen the singer and ask Him to fight against those who oppose them. The song reflects on how enemies misunderstood the singer's relationship with God and rejoiced in their troubles, but God arose in response. It references Christ's sacrifice, stating that He was beaten and mocked so that the believer could be blessed and honored. The overall message is one of trust in God's faithfulness and victory over adversaries.

Lyrics Verified by Editorial Team

Wewe ni Mungu uliyenichagua 

Naomba pigana nao wanaopigana nami 

Wewe ni Mungu uliyenichagua 

Naomba pigana nao wanaopigana nami 


Hawakujua kama ni Baba 

Hawakujua kama wewe ni Baba 

Hawakujua mimi ni mboni la jicho lako 

Hawakujua nimechorwa viganjani mwako 

Hawakujua ulipigwa kwa ajili yangu Baba 

Hawakujua ulichibuliwa kwa ajili yangu

Hawakujua ulifanyika laana nifanyike baraka

Hawakujua ulidhihakiwa kwa ajili yangu 

Hawakujua ulidhihakiwa ili niheshimiwe 

Hawakujua ulipigwa kwa ajili yangu Yesu 

Wafadhaishe hao warudishwe nyuma hao 

Warudishwe nyuma yangu 


Wewe ni Mungu uliyenichagua 

Naomba pigana nao wanaopigana nami 

Wewe ni Mungu uliyenichagua 

Naomba pigana nao wanaopigana nami 


Wapenzi wa misiba wangu maadui wanichekelea 

Wakati wa misiba yangu maadui walifurahi 

Wakati wa kufiwa kwangu waliweka vikao vyao 

Wakadhani Mungu wangu umeniacha 

Wakadhani Mungu wangu umenisahau 

Wakadhani Mungu wangu umenikimbia 

Kumbe maneno yao yakafanya ukainuka 

Masengenyo yao vikao vyao vikafanya uamke 

Wacha niimbe wewe ni Mungu 

Wewe ni Mungu uliyenichagua 

Naomba pigana nao wanaopigana nami 


Wewe ni Mungu uliyenichagua 

Naomba pigana nao wanaopigana nami 

Wewe ni Mungu uliyenichagua 

Naomba pigana nao wanaopigana nami 

Music Video

Save Your Favorites

Create a free account to save songs, build your personal library, and connect with the Zion community.

Create Free Account

Join the Zion Community

Create a free account to save your favorite lyrics, submit song suggestions, and connect with fellow worshippers.

No spam. Unsubscribe anytime.