2 Mambo ya Nyakati Mlango 16 2nd Chronicles

2 Mambo ya Nyakati 16:1 2ndChronicles 16:1

Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwake Asa, Baasha mfalme wa Israeli akapanda juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu ye yote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.

2 Mambo ya Nyakati 16:2 2ndChronicles 16:2

Ndipo Asa akatoa fedha na dhahabu katika hazina za nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, akampelekea Ben-hadadi mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema,

2 Mambo ya Nyakati 16:3 2ndChronicles 16:3

Kwangu na kwako na liwe agano kama lilivyokuwa kwa baba yangu na baba yako; angalia, nimekuletea fedha na dhahabu; basi, uvunje agano lako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili aniondokee mimi.

2 Mambo ya Nyakati 16:4 2ndChronicles 16:4

Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawapeleka maakida wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli; wakapiga Iyoni, na Dani, na Abel-maimu, na miji ya hazina yote ya Naftali.

2 Mambo ya Nyakati 16:5 2ndChronicles 16:5

Ikawa Baasha aliposikia habari hiyo, akaacha kuujenga Rama, akaikomesha kazi yake.

2 Mambo ya Nyakati 16:6 2ndChronicles 16:6

Ndipo mfalme Asa akawatwaa Yuda wote; nao wakayachukua mawe ya Rama, na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye akajenga kwa vitu hivyo Geba na Mispa.

2 Mambo ya Nyakati 16:7 2ndChronicles 16:7

Wakati ule Hanani mwonaji akamwendea Asa mfalme wa Yuda, akamwambia, Kwa kuwa umemtegemea mfalme wa Shamu, wala hukumtegemea Bwana, Mungu wako, kwa hiyo limeokoka jeshi la mfalme wa Shamu mkononi mwako.

2 Mambo ya Nyakati 16:8 2ndChronicles 16:8

Je! Hao Wakushi na Walubi hawakuwa jeshi kubwa mno, wenye magari na wapanda farasi wengi sana? Lakini, kwa kuwa ulimtegemea Bwana, aliwatia mkononi mwako.

2 Mambo ya Nyakati 16:9 2ndChronicles 16:9

Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.

2 Mambo ya Nyakati 16:10 2ndChronicles 16:10

Ndipo Asa akamkasirikia mwonaji, akamtia nyumbani mwa mkatale; maana amemghadhibikia kwa sababu ya neno hilo. Na Asa akawaonea baadhi ya watu wakati ule ule.

2 Mambo ya Nyakati 16:11 2ndChronicles 16:11

Na tazama, mambo yake Asa, ya kwanza na ya mwisho, angalia, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.

2 Mambo ya Nyakati 16:12 2ndChronicles 16:12

Akashikwa Asa na ugonjwa wa miguu katika mwaka wa thelathini na kenda wa kumiliki kwake; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta Bwana katika ugonjwa wake, bali waganga.

2 Mambo ya Nyakati 16:13 2ndChronicles 16:13

Asa akalala na babaze, akafa katika mwaka wa arobaini na mmoja wa kumiliki kwake.

2 Mambo ya Nyakati 16:14 2ndChronicles 16:14

Wakamzika katika makaburi yake mwenyewe, aliyojichimbia katika mji wa Daudi, wakamlaza juu ya kitanda kilichojazwa manukato, na kila namna ya machanganyiko ya hao mafundi wa dawa; wakamfukizia mafukizo makuu sana.