2 Mambo ya Nyakati Mlango 33 2nd Chronicles

2 Mambo ya Nyakati 33:1 2ndChronicles 33:1

Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka hamsini na mitano.

2 Mambo ya Nyakati 33:2 2ndChronicles 33:2

Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, sawasawa na machukizo yote ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli.

2 Mambo ya Nyakati 33:3 2ndChronicles 33:3

Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopabomoa Hezekia babaye; akazisimamisha madhabahu za mabaali, akafanya na sanamu za maashera, akaabudu jeshi lote la mbinguni, na kulitumikia.

2 Mambo ya Nyakati 33:4 2ndChronicles 33:4

Akajenga madhabahu katika nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu litakuwako jina langu milele.

2 Mambo ya Nyakati 33:5 2ndChronicles 33:5

Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika nyua mbili za nyumba ya Bwana.

2 Mambo ya Nyakati 33:6 2ndChronicles 33:6

Tena akawapitisha wanawe motoni katika bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.

2 Mambo ya Nyakati 33:7 2ndChronicles 33:7

Akaiweka sanamu ya kuchonga aliyoifanya, katika nyumba ya Mungu ambayo Mungu alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele;

2 Mambo ya Nyakati 33:8 2ndChronicles 33:8

wala sitawaondoshea miguu tena Israeli katika nchi niliyowaagizia baba zenu; wakiangalia tu kutenda yote niliyowaamuru, yaani, torati yote, na sheria, na maagizo, niliyowaamuru kwa mkono wa Musa.

2 Mambo ya Nyakati 33:9 2ndChronicles 33:9

Basi Manase akawakosesha Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, hata wakazidi kufanya mabaya kuliko mataifa, aliowaharibu Bwana mbele ya wana wa Israeli.

2 Mambo ya Nyakati 33:10 2ndChronicles 33:10

Naye Bwana akasema na Manase, na watu wake; wala wasiangalie.

2 Mambo ya Nyakati 33:11 2ndChronicles 33:11

Kwa hiyo Bwana akaleta juu yao maakida wa jeshi la mfalme wa Ashuru, waliomkamata Manase kwa minyororo, wakamfunga kwa pingu, wakamchukua mpaka Babeli.

2 Mambo ya Nyakati 33:12 2ndChronicles 33:12

Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi Bwana, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake.

2 Mambo ya Nyakati 33:13 2ndChronicles 33:13

Akamwomba; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba Bwana ndiye Mungu.

2 Mambo ya Nyakati 33:14 2ndChronicles 33:14

Hata baada ya hayo akaujengea mji wa Daudi ukuta wa nje, upande wa magharibi wa Gihoni, bondeni, hata kufika maingilio ya lango la samaki; akauzungusha Ofeli, akauinua juu sana; akaweka maakida mashujaa katika miji yote ya Yuda yenye maboma.

2 Mambo ya Nyakati 33:15 2ndChronicles 33:15

Akaiondoa miungu migeni, na hiyo sanamu nyumbani mwa Bwana, na madhabahu zote alizozijenga katika mlima wa nyumba ya Bwana, na Yerusalemu, akazitupa nje ya mji.

2 Mambo ya Nyakati 33:16 2ndChronicles 33:16

Akaijenga madhabahu ya Bwana, akatoa juu yake dhabihu za sadaka za amani, na za shukrani, akawaamuru Yuda wamtumikie Bwana, Mungu wa Israeli.

2 Mambo ya Nyakati 33:17 2ndChronicles 33:17

Lakini watu wakaendelea kutoa dhabihu katika mahali pa juu, ila wakamtolea Bwana, Mungu wao tu.

2 Mambo ya Nyakati 33:18 2ndChronicles 33:18

Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji walionena naye kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa kati ya mambo ya wafalme wa Israeli.

2 Mambo ya Nyakati 33:19 2ndChronicles 33:19

Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika tarehe ya Hozai.

2 Mambo ya Nyakati 33:20 2ndChronicles 33:20

Basi Manase akalala na babaze, wakamzika nyumbani mwake; na Amoni mwanawe akatawala mahali pake.

2 Mambo ya Nyakati 33:21 2ndChronicles 33:21

Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka miwili.

2 Mambo ya Nyakati 33:22 2ndChronicles 33:22

Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, kama alivyofanya Manase babaye; Amoni akazitolea dhabihu sanamu zote alizozifanya Manase babaye, akazitumikia.

2 Mambo ya Nyakati 33:23 2ndChronicles 33:23

Wala hakujinyenyekeza mbele za Bwana, kama Manase babaye alivyojinyenyekeza; lakini huyo Amoni akaongeza makosa juu ya makosa.

2 Mambo ya Nyakati 33:24 2ndChronicles 33:24

Wakamfanyia fitina watumishi wake, wakamwua katika nyumba yake mwenyewe.

2 Mambo ya Nyakati 33:25 2ndChronicles 33:25

Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliomfanyia fitina mfalme Amoni; watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme badala yake.