2 Wafalme Mlango 11 2nd Kings

2 Wafalme 11:1 2ndKings 11:1

Na Athalia, mama yake Ahazia, alipoona ya kuwa mwanawe amekufa, akainuka, akawaharibu wazao wote wa kifalme.

2 Wafalme 11:2 2ndKings 11:2

Ila Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu, umbu lake Ahazia ,akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia ,akamwiba miongoni mwa hao wana wa mfalme waliouawa ,yeye na mlezi wake ,na kuwatia katika chumba cha kulala;wakamficha usoni pa Athalia,basi kwa hiyo hakuuawa.

2 Wafalme 11:3 2ndKings 11:3

Alikuwako pamoja naye, amefichwa nyumbani mwa Bwana, miaka sita. Naye Athalia akaitawala nchi.

2 Wafalme 11:4 2ndKings 11:4

Hata mwaka wa saba Yehoyada akatuma, na kuwaleta wakuu wa mamia, wa Wakari, na wa walinzi, akawaleta kwake ndani ya nyumba ya Bwana; akapatana nao, akawaapisha nyumbani mwa Bwana, akawaonyesha huyo mwana wa mfalme.

2 Wafalme 11:5 2ndKings 11:5

Akawaamuru, akasema, Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi yenu, mtakaoingia siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya mfalme;

2 Wafalme 11:6 2ndKings 11:6

na theluthi mtakuwapo mlangoni pa Suri; na theluthi langoni nyuma ya walinzi; hivyo mtayalinda malinzi ya nyumba, kuzuia watu wasiingie.

2 Wafalme 11:7 2ndKings 11:7

Na sehemu mbili zenu, yaani, wote watokao siku ya sabato, mtayalinda malinzi ya nyumba ya Bwana kumzunguka mfalme.

2 Wafalme 11:8 2ndKings 11:8

Mtamzunguka mfalme pande zote, kila mtu mwenye silaha zake mkononi; naye awaye yote aingiaye ndani ya safu auawe; mkafuatane na mfalme, akitoka na akiingia.

2 Wafalme 11:9 2ndKings 11:9

Nao wakuu wa mamia wakafanya sawasawa na yote aliyowaamuru Yehoyada kuhani; wakawatwaa kila mtu watu wake, hao watakaoingia sabato, nao watakaotoka sabato, wakaja kwa Yehoyada kuhani.

2 Wafalme 11:10 2ndKings 11:10

Naye yule kuhani akawapa wakuu wa mamia mikuki na ngao zilizokuwa za mfalme Daudi, zilizokuwamo nyumbani mwa Bwana.

2 Wafalme 11:11 2ndKings 11:11

Walinzi wakasimama, kila mtu na silaha zake mkononi, kutoka pembe ya kuume ya nyumba mpaka pembe ya kushoto ya nyumba, kando ya madhabahu na nyumba, wakimzunguka mfalme pande zote.

2 Wafalme 11:12 2ndKings 11:12

Ndipo akamleta nje mwana wa mfalme, akamvika taji, na kumpa ushuhuda; wakamfanya mfalme, wakamtia mafuta; wakapiga makofi, wakasema, mfalme na aishi.

2 Wafalme 11:13 2ndKings 11:13

Na Athalia alipoisikia sauti ya walinzi na ya watu, aliingia kwa watu nyumbani kwa Bwana;

2 Wafalme 11:14 2ndKings 11:14

akatazama, na tazama, mfalme amesimama karibu na nguzo kama ilivyokuwa desturi, nao wakuu na wapiga baragumu karibu na mfalme; na watu wote wa nchi wakafurahi, wakapiga baragumu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akalia, Fitina! Fitina!

2 Wafalme 11:15 2ndKings 11:15

Naye Yehoyada kuhani akawaamuru wakuu wa mamia, majemadari wa jeshi, akawaambia, Mtoeni kati ya safu; naye ye yote amfuataye mwueni kwa upanga. Kwani kuhani akasema, Asiuawe nyumbani mwa Bwana.

2 Wafalme 11:16 2ndKings 11:16

Basi wakampisha njia; akaenda kwa njia ya kuingia kwa farasi nyumbani mwa mfalme; akauawa huko.

2 Wafalme 11:17 2ndKings 11:17

Kisha, Yehoyada akafanya mapatano kati ya Bwana na mfalme na watu, ili wawe watu wa Bwana; tena kati ya mfalme na watu.

2 Wafalme 11:18 2ndKings 11:18

Watu wote wa nchi wakaiendea nyumba ya Baali, wakaiangusha; madhabahu zake na sanamu zake wakazivunja-vunja kabisa, na Matani kuhani wa Baali wakamwua mbele ya madhabahu. Na Yehoyada kuhani akaweka maakida juu ya nyumba ya Bwana.

2 Wafalme 11:19 2ndKings 11:19

Akawatwaa wakuu wa mamia, na Wakari, na walinzi, na watu wote wa nchi; wakamleta mfalme kushuka nyumbani mwa Bwana, wakaja kwa njia ya mlango wa walinzi mpaka nyumba ya mfalme. Naye akakaa katika kiti cha enzi cha wafalme.

2 Wafalme 11:20 2ndKings 11:20

Basi watu wote wa nchi wakafurahi, na mji ukatulia. Naye Athalia wakamwua kwa upanga karibu na nyumba ya mfalme.

2 Wafalme 11:21 2ndKings 11:21

Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala.