2 Wafalme Mlango 12 2nd Kings

2 Wafalme 12:1 2ndKings 12:1

Katika mwaka wa saba wa Yehu, Yoashi alianza kutawala; akatawala miaka arobaini huko Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Sibia wa Beer-sheba.

2 Wafalme 12:2 2ndKings 12:2

Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana siku zake zote Yehoyada kuhani alizomfundisha.

2 Wafalme 12:3 2ndKings 12:3

Ila mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.

2 Wafalme 12:4 2ndKings 12:4

Yoashi akawaambia makuhani, Fedha yote ya vitu vitakatifu iliyoletwa nyumbani mwa Bwana, fedha ya matumizi, fedha ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na fedha yote iliyoletwa kama mtu ye yote aonavyo moyoni mwake kuileta nyumbani mwa Bwana,

2 Wafalme 12:5 2ndKings 12:5

makuhani na waitwae, kila mtu kwa hao awajuao; nao watatengeneza palipobomoka nyumbani, kila mahali palipoonekana pamebomoka.

2 Wafalme 12:6 2ndKings 12:6

Lakini ikawa, mwaka wa ishirini na tatu wa mfalme Yoashi, makuhani walikuwa hawajatengeneza mabomoko ya nyumba.

2 Wafalme 12:7 2ndKings 12:7

Ndipo mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani, na makuhani wengine, akawauliza, Mbona hamtengenezi mabomoko ya nyumba? Basi sasa msipokee tena fedha kwa hao mwajuao, lakini itoeni kwa ajili ya mabomoko ya nyumba.

2 Wafalme 12:8 2ndKings 12:8

Nao makuhani wakakubali kwamba wasipokee fedha kwa watu, wala wasitengeneze mabomoko ya nyumba.

2 Wafalme 12:9 2ndKings 12:9

Lakini Yehoyada kuhani akatwaa kasha, akatoboa tundu katika kifuniko chake, akaliweka karibu na madhabahu, upande wa kuume mtu aingiapo nyumbani mwa Bwana; na makuhani, waliolinda mlangoni, wakatia ndani yake fedha yote iliyoletwa nyumbani mwa Bwana.

2 Wafalme 12:10 2ndKings 12:10

Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa Bwana.

2 Wafalme 12:11 2ndKings 12:11

Na fedha iliyopimwa wakawapa mikononi wale waliofanya kazi, walioisimamia nyumba ya Bwana; na hao wakawatolea maseremala na wajenzi walioifanya kazi katika nyumba ya Bwana,

2 Wafalme 12:12 2ndKings 12:12

na hao waashi, na wakata mawe, tena kununua miti na mawe ya kuchongwa, ili kuyatengeneza mabomoko ya nyumba ya Bwana, tena kwa gharama zote za kuitengeneza nyumba.

2 Wafalme 12:13 2ndKings 12:13

Lakini havikufanywa kwa nyumba ya Bwana vikombe vya fedha, wala makasi, wala mabakuli, wala panda, wala vyombo vyo vyote vya dhahabu, wala vyombo vya fedha, kwa hiyo fedha iliyoletwa nyumbani mwa Bwana;

2 Wafalme 12:14 2ndKings 12:14

kwa sababu hiyo fedha waliwapa watenda kazi, wakaitengeneza kwayo nyumba ya Bwana.

2 Wafalme 12:15 2ndKings 12:15

Walakini hawakufanya hesabu na hao watu, waliokabidhiwa fedha hiyo ili wawape watenda kazi; kwa kuwa walitenda kwa uaminifu.

2 Wafalme 12:16 2ndKings 12:16

Lakini fedha ya matoleo ya kosa, na fedha ya matoleo ya dhambi, haikuletwa nyumbani mwa Bwana; hiyo ilikuwa ya makuhani wenyewe.

2 Wafalme 12:17 2ndKings 12:17

Ndipo akakwea Hazaeli mfalme wa Shamu akapigana na Gathi, akautwaa; Hazaeli akaelekeza uso ili akwee kwenda Yerusalemu.

2 Wafalme 12:18 2ndKings 12:18

Yoashi mfalme wa Yuda akavitwaa vyote alivyoviweka wakfu Yehoshafati, na Yehoramu, na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, navyo vyote alivyoweka wakfu mwenyewe, na dhahabu yote iliyoonekana katika hazina za nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, akamletea Hazaeli mfalme wa Shamu; basi akaenda zake kutoka Yerusalemu.

2 Wafalme 12:19 2ndKings 12:19

Basi mambo yote ya Yoashi yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?

2 Wafalme 12:20 2ndKings 12:20

Nao watumishi wake wakaondoka, wakafanya fitina, wakamwua Yoashi katika nyumba ya Milo, hapo panaposhukia Sila.

2 Wafalme 12:21 2ndKings 12:21

Kwa maana Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakampiga, naye akafa; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.