2 Wafalme Mlango 20 2nd Kings

2 Wafalme 20:1 2ndKings 20:1

Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

2 Wafalme 20:2 2ndKings 20:2

Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana akasema,

2 Wafalme 20:3 2ndKings 20:3

Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.

2 Wafalme 20:4 2ndKings 20:4

Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia, kusema,

2 Wafalme 20:5 2ndKings 20:5

Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.

2 Wafalme 20:6 2ndKings 20:6

Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.

2 Wafalme 20:7 2ndKings 20:7

Naye Isaya akasema, Twaeni mkate wa tini. Wakautwaa, wakauweka juu ya jipu, naye akapona.

2 Wafalme 20:8 2ndKings 20:8

Hezekia akamwambia Isaya, Je! Kutakuwa na ishara gani ya kwamba Bwana ataniponya, nami siku ya tatu nitapanda nyumbani kwa Bwana.

2 Wafalme 20:9 2ndKings 20:9

Isaya akamwambia, Jambo hili litakuwa ishara kwako, itokayo kwa Bwana, ya kwamba Bwana atalifanya neno hilo alilolinena; je! Kivuli kiendelee madaraja kumi, au kirudi nyuma madaraja kumi?

2 Wafalme 20:10 2ndKings 20:10

Hezekia akajibu, Ni jambo jepesi kivuli kuendelea madaraja kumi; la, hicho kivuli na kirudi nyuma madaraja kumi.

2 Wafalme 20:11 2ndKings 20:11

Isaya nabii akamlilia Bwana; akakirudisha nyuma kile kivuli madaraja kumi, ambayo kilikuwa kimeshuka katika madaraja ya Ahazi.

2 Wafalme 20:12 2ndKings 20:12

Wakati huo Merodak-baladani mwana wa Baladani, Mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana alipata habari kwamba Hezekia ameugua.

2 Wafalme 20:13 2ndKings 20:13

Hezekia akawasikiliza, akawaonyesha nyumba yote yenye vitu vyake vya thamani, fedha, na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yenye silaha zake, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake. Wala hapakuwa na kitu asichowaonyesha Hezekia, katika nyumba yake, wala katika ufalme wake wote.

2 Wafalme 20:14 2ndKings 20:14

Ndipo Isaya nabii akamwendea mfalme Hezekia, akamwambia, Wasemaje watu hawa? Nao wametoka wapi kuja kwako? Hezekia akasema, Wametoka katika nchi iliyo mbali, yaani Babeli.

2 Wafalme 20:15 2ndKings 20:15

Ndipo akasema, Wameona nini nyumbani mwako? Hezekia akajibu, Vitu vyote vilivyomo nyumbani mwangu wameviona; hapana kitu nisichowaonyesha katika hazina zangu.

2 Wafalme 20:16 2ndKings 20:16

Isaya akamwambia Hezekia, Basi, lisikie neno la Bwana,

2 Wafalme 20:17 2ndKings 20:17

Angalia, siku zinakuja, ambazo vitu vyote vilivyomo nyumbani mwako, na hivyo vilivyowekwa akiba na baba zako hata leo, vitachukuliwa mpaka Babeli; hakitasalia kitu, asema Bwana.

2 Wafalme 20:18 2ndKings 20:18

Na baadhi ya wanao watakaotoka kwako, utakaowazaa, watawachukulia mbali; nao watakuwa matowashi jumbani mwake mfalme wa Babeli.

2 Wafalme 20:19 2ndKings 20:19

Ndipo Hezekia akamwambia Isaya, Neno la Bwana ulilolinena ni jema. Tena akasema, Je! Sivyo, ikiwapo amani na kweli katika siku zangu?

2 Wafalme 20:20 2ndKings 20:20

Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na ushujaa wake wote, tena alivyolifanya birika na mfereji, akaleta maji ndani ya mji, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?

2 Wafalme 20:21 2ndKings 20:21

Hezekia akalala na baba zake; na Manase mwanawe akatawala mahali pake.