1 Mambo ya Nyakati Mlango 27 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 27:1 1stChronicles 27:1

Basi wana wa Israeli kwa hesabu yao, wakuu wa mbari za mababa, na maakida wa maelfu na wa mamia, na wasimamizi wao waliomtumikia mfalme, kwa neno lo lote la zamu za kuingia na za kutoka mwezi kwa mwezi, miezi yote ya mwaka, wa kila zamu, walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:2 1stChronicles 27:2

Juu ya zamu ya kwanza ya mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu, mwana wa Zabdieli; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:3 1stChronicles 27:3

Yeye alikuwa wa wana wa Peresi, mkuu wa maakida wote wa jeshi mwezi wa kwanza.

1 Mambo ya Nyakati 27:4 1stChronicles 27:4

Na juu ya zamu ya mwezi wa pili alikuwa Dodai, Mwahohi, na zamu yake; na Miklothi alikuwa amiri; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:5 1stChronicles 27:5

Akida wa tatu wa jeshi mwezi wa tatu alikuwa Benaya, mwana wa Yehoyada, kuhani; alikuwa mkuu, na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:6 1stChronicles 27:6

Huyo Benaya ndiye yule aliyekuwa shujaa wa wale thelathini, na juu ya wale thelathini; na katika zamu yake alikuwa Amizabadi mwanawe.

1 Mambo ya Nyakati 27:7 1stChronicles 27:7

Akida wa nne wa mwezi wa nne alikuwa Asaheli, nduguye Yoabu, na Zebadia mwanawe baada yake; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:8 1stChronicles 27:8

Akida wa tano wa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi, Mwizrahi; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:9 1stChronicles 27:9

Akida wa sita wa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:10 1stChronicles 27:10

Akida wa saba wa mwezi wa saba alikuwa Heksi, Mpeloni, wa wana wa Efraimu; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:11 1stChronicles 27:11

Akida wa nane wa mwezi wa nane alikuwa Sibekai, Mhushathi, wa Wazera; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:12 1stChronicles 27:12

Akida wa kenda wa mwezi wa kenda alikuwa Abiezeri, Mwanathothi, wa Wabenyamini; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:13 1stChronicles 27:13

Akida wa kumi wa mwezi wa kumi alikuwa Maharai, Mnetofathi, wa Wazera; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:14 1stChronicles 27:14

Akida wa kumi na moja wa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya, Mpirathoni, wa wana wa Efraimu; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:15 1stChronicles 27:15

Akida wa kumi na mbili wa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heledi, Mnetofathi, wa Othnieli; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

1 Mambo ya Nyakati 27:16 1stChronicles 27:16

Tena wakuu wa kabila za Israeli walikuwa hawa; wa Wareubeni, Eliezeri mwana wa Zikri; wa Wasimeoni, Shefatia mwana wa Maaka;

1 Mambo ya Nyakati 27:17 1stChronicles 27:17

wa Lawi, Hashabia mwana wa Kemueli; wa Haruni, Sadoki;

1 Mambo ya Nyakati 27:18 1stChronicles 27:18

wa Yuda, Elihu, mmojawapo wa nduguze Daudi; wa Isakari, Omri mwana wa Mikaeli;

1 Mambo ya Nyakati 27:19 1stChronicles 27:19

wa Zabuloni, Ishmaya mwana wa Obadia; wa Naftali, Yeromothi mwana wa Azrieli;

1 Mambo ya Nyakati 27:20 1stChronicles 27:20

wa wana wa Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia, wa nusu kabila ya Manase, Yoeli mwana wa Pedaya;

1 Mambo ya Nyakati 27:21 1stChronicles 27:21

wa nusu kabila ya Manase katika Gileadi, Ido mwana wa Zekaria; wa Benyamini, Yaasieli mwana wa Abneri;

1 Mambo ya Nyakati 27:22 1stChronicles 27:22

wa Dani, Azareli mwana wa Yerohamu. Hao walikuwa maakida wa kabila za Israeli.

1 Mambo ya Nyakati 27:23 1stChronicles 27:23

Lakini Daudi hakufanya hesabu yao wenye miaka ishirini na waliopungua; kwa kuwa Bwana alikuwa amesema, ya kwamba atawaongeza Israeli mfano wa nyota za mbinguni.

1 Mambo ya Nyakati 27:24 1stChronicles 27:24

Yoabu, mwana wa Seruya, akaanza kuhesabu, lakini hakumaliza; na ghadhabu ikawapata Israeli kwa hayo; wala haikuhesabiwa hesabu hiyo ndani ya taarifa za mfalme Daudi.

1 Mambo ya Nyakati 27:25 1stChronicles 27:25

Na juu ya hazina za mfalme alikuwa Azmawethi mwana wa Adieli; na juu ya hazina za mashambani, za mijini, na vijijini, na ngomeni, alikuwa Yonathani mwana wa Uzia;

1 Mambo ya Nyakati 27:26 1stChronicles 27:26

na juu ya hao wenye kazi ya shamba kuilima ardhi alikuwa Ezri mwana wa Kelubu;

1 Mambo ya Nyakati 27:27 1stChronicles 27:27

na juu ya mashamba ya mizabibu alikuwa Shimei, Mramathi; na juu ya mazao ya mizabibu kwa ghala za mvinyo alikuwa Zabdi, Mshifmi;

1 Mambo ya Nyakati 27:28 1stChronicles 27:28

na juu ya mizeituni na mikuyu iliyokuwamo katika Shefela alikuwa Baal-hanani, Mgederi; na juu ya ghala za mafuta alikuwa Yoashi;

1 Mambo ya Nyakati 27:29 1stChronicles 27:29

na juu ya makundi ya ng'ombe waliolishwa katika Sharoni alikuwa Shitrai, Msharoni; na juu ya makundi waliokuwamo mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai;

1 Mambo ya Nyakati 27:30 1stChronicles 27:30

na juu ya ngamia alikuwa Obili, Mwishmaeli; na juu ya punda alikuwa Yedeya, Mmeronothi;

1 Mambo ya Nyakati 27:31 1stChronicles 27:31

na juu ya makundi ya kondoo alikuwa Yazizi, Mhagri. Hao wote walikuwa maakida wa akiba alizokuwa nazo mfalme Daudi.

1 Mambo ya Nyakati 27:32 1stChronicles 27:32

Naye Yonathani, mjombawe Daudi, alikuwa mshauri, na mtu wa akili, na mwandishi; Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa pamoja na wana wa mfalme;

1 Mambo ya Nyakati 27:33 1stChronicles 27:33

na Ahithofeli alikuwa mshauri wake mfalme; na Hushai, Mwarki, alikuwa rafiki yake mfalme;

1 Mambo ya Nyakati 27:34 1stChronicles 27:34

na, baada ya Ahithofeli, walikuwa Yehoyada mwana wa Benaya, na Abiathari; na jemadari wa jeshi la mfalme alikuwa Yoabu.