1 Wakorintho Mlango 10 1st Corinthians

1 Wakorintho 10:1 1stCorinthians 10:1

Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;

1 Wakorintho 10:2 1stCorinthians 10:2

wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;

1 Wakorintho 10:3 1stCorinthians 10:3

wote wakala chakula kile kile cha roho;

1 Wakorintho 10:4 1stCorinthians 10:4

wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.

1 Wakorintho 10:5 1stCorinthians 10:5

Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.

1 Wakorintho 10:6 1stCorinthians 10:6

Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.

1 Wakorintho 10:7 1stCorinthians 10:7

Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.

1 Wakorintho 10:8 1stCorinthians 10:8

Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.

1 Wakorintho 10:9 1stCorinthians 10:9

Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.

1 Wakorintho 10:10 1stCorinthians 10:10

Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu.

1 Wakorintho 10:11 1stCorinthians 10:11

Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

1 Wakorintho 10:12 1stCorinthians 10:12

Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.

1 Wakorintho 10:13 1stCorinthians 10:13

Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

1 Wakorintho 10:14 1stCorinthians 10:14

Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.

1 Wakorintho 10:15 1stCorinthians 10:15

Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo.

1 Wakorintho 10:16 1stCorinthians 10:16

Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?

1 Wakorintho 10:17 1stCorinthians 10:17

Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.

1 Wakorintho 10:18 1stCorinthians 10:18

Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu?

1 Wakorintho 10:19 1stCorinthians 10:19

Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?

1 Wakorintho 10:20 1stCorinthians 10:20

Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.

1 Wakorintho 10:21 1stCorinthians 10:21

Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.

1 Wakorintho 10:22 1stCorinthians 10:22

Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?

1 Wakorintho 10:23 1stCorinthians 10:23

Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.

1 Wakorintho 10:24 1stCorinthians 10:24

Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake.

1 Wakorintho 10:25 1stCorinthians 10:25

Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri;

1 Wakorintho 10:26 1stCorinthians 10:26

maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.

1 Wakorintho 10:27 1stCorinthians 10:27

Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.

1 Wakorintho 10:28 1stCorinthians 10:28

Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri.

1 Wakorintho 10:29 1stCorinthians 10:29

Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?

1 Wakorintho 10:30 1stCorinthians 10:30

Ikiwa mimi natumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho?

1 Wakorintho 10:31 1stCorinthians 10:31

Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

1 Wakorintho 10:32 1stCorinthians 10:32

Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu,

1 Wakorintho 10:33 1stCorinthians 10:33

vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.