1 Wakorintho Mlango 16 1st Corinthians

1 Wakorintho 16:1 1stCorinthians 16:1

Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.

1 Wakorintho 16:2 1stCorinthians 16:2

Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;

1 Wakorintho 16:3 1stCorinthians 16:3

nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu.

1 Wakorintho 16:4 1stCorinthians 16:4

Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami.

1 Wakorintho 16:5 1stCorinthians 16:5

Lakini nitakuja kwenu, nikiisha kupita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia.

1 Wakorintho 16:6 1stCorinthians 16:6

Labda nitakaa kwenu; naam, labda wakati wote wa baridi, mpate kunisafirisha ko kote nitakakokwenda.

1 Wakorintho 16:7 1stCorinthians 16:7

Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraji kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia.

1 Wakorintho 16:8 1stCorinthians 16:8

Lakini nitakaa Efeso hata Pentekoste;

1 Wakorintho 16:9 1stCorinthians 16:9

kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.

1 Wakorintho 16:10 1stCorinthians 16:10

Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo hofu; maana anaifanya kazi ya Bwana vile vile kama mimi mwenyewe;

1 Wakorintho 16:11 1stCorinthians 16:11

basi mtu ye yote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, ili aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu.

1 Wakorintho 16:12 1stCorinthians 16:12

Lakini kwa habari za Apolo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja na hao ndugu; ambaye si mapenzi yake kwenda sasa; lakini atakuja atakapopata nafasi.

1 Wakorintho 16:13 1stCorinthians 16:13

Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.

1 Wakorintho 16:14 1stCorinthians 16:14

Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.

1 Wakorintho 16:15 1stCorinthians 16:15

Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni malimbuko ya Akaya, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu);

1 Wakorintho 16:16 1stCorinthians 16:16

watiini watu kama hawa, na kila mtu afanyaye kazi pamoja nao, na kujitaabisha.

1 Wakorintho 16:17 1stCorinthians 16:17

Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu.

1 Wakorintho 16:18 1stCorinthians 16:18

Maana wameniburudisha roho yangu, na roho zenu pia; basi wajueni sana watu kama hao.

1 Wakorintho 16:19 1stCorinthians 16:19

Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao.

1 Wakorintho 16:20 1stCorinthians 16:20

Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.

1 Wakorintho 16:21 1stCorinthians 16:21

Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe.

1 Wakorintho 16:22 1stCorinthians 16:22

Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha.

1 Wakorintho 16:23 1stCorinthians 16:23

Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi.

1 Wakorintho 16:24 1stCorinthians 16:24

Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu.