1 Wakorintho Mlango 6 1st Corinthians

1 Wakorintho 6:1 1stCorinthians 6:1

Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?

1 Wakorintho 6:2 1stCorinthians 6:2

Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?

1 Wakorintho 6:3 1stCorinthians 6:3

Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?

1 Wakorintho 6:4 1stCorinthians 6:4

Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa?

1 Wakorintho 6:5 1stCorinthians 6:5

Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake?

1 Wakorintho 6:6 1stCorinthians 6:6

Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao wasioamini.

1 Wakorintho 6:7 1stCorinthians 6:7

Basi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang'anywa mali zenu?

1 Wakorintho 6:8 1stCorinthians 6:8

Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang'anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu.

1 Wakorintho 6:9 1stCorinthians 6:9

Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,

1 Wakorintho 6:10 1stCorinthians 6:10

wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.

1 Wakorintho 6:11 1stCorinthians 6:11

Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.

1 Wakorintho 6:12 1stCorinthians 6:12

Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.

1 Wakorintho 6:13 1stCorinthians 6:13

Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.

1 Wakorintho 6:14 1stCorinthians 6:14

Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.

1 Wakorintho 6:15 1stCorinthians 6:15

Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!

1 Wakorintho 6:16 1stCorinthians 6:16

Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.

1 Wakorintho 6:17 1stCorinthians 6:17

Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.

1 Wakorintho 6:18 1stCorinthians 6:18

Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.

1 Wakorintho 6:19 1stCorinthians 6:19

Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

1 Wakorintho 6:20 1stCorinthians 6:20

maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.