1 Wakorintho Mlango 13 1st Corinthians

1 Wakorintho 13:1 1stCorinthians 13:1

Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

1 Wakorintho 13:2 1stCorinthians 13:2

Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

1 Wakorintho 13:3 1stCorinthians 13:3

Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

1 Wakorintho 13:4 1stCorinthians 13:4

Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

1 Wakorintho 13:5 1stCorinthians 13:5

haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

1 Wakorintho 13:6 1stCorinthians 13:6

haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

1 Wakorintho 13:7 1stCorinthians 13:7

huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

1 Wakorintho 13:8 1stCorinthians 13:8

Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

1 Wakorintho 13:9 1stCorinthians 13:9

Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;

1 Wakorintho 13:10 1stCorinthians 13:10

lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.

1 Wakorintho 13:11 1stCorinthians 13:11

Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.

1 Wakorintho 13:12 1stCorinthians 13:12

Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.

1 Wakorintho 13:13 1stCorinthians 13:13

Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.