1 Wakorintho Mlango 15 1st Corinthians

1 Wakorintho 15:1 1stCorinthians 15:1

Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama,

1 Wakorintho 15:2 1stCorinthians 15:2

na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure.

1 Wakorintho 15:3 1stCorinthians 15:3

Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;

1 Wakorintho 15:4 1stCorinthians 15:4

na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;

1 Wakorintho 15:5 1stCorinthians 15:5

na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara;

1 Wakorintho 15:6 1stCorinthians 15:6

baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;

1 Wakorintho 15:7 1stCorinthians 15:7

baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote;

1 Wakorintho 15:8 1stCorinthians 15:8

na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.

1 Wakorintho 15:9 1stCorinthians 15:9

Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.

1 Wakorintho 15:10 1stCorinthians 15:10

Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.

1 Wakorintho 15:11 1stCorinthians 15:11

Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini.

1 Wakorintho 15:12 1stCorinthians 15:12

Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?

1 Wakorintho 15:13 1stCorinthians 15:13

Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka;

1 Wakorintho 15:14 1stCorinthians 15:14

tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.

1 Wakorintho 15:15 1stCorinthians 15:15

Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.

1 Wakorintho 15:16 1stCorinthians 15:16

Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.

1 Wakorintho 15:17 1stCorinthians 15:17

Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.

1 Wakorintho 15:18 1stCorinthians 15:18

Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.

1 Wakorintho 15:19 1stCorinthians 15:19

Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.

1 Wakorintho 15:20 1stCorinthians 15:20

Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.

1 Wakorintho 15:21 1stCorinthians 15:21

Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.

1 Wakorintho 15:22 1stCorinthians 15:22

Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.

1 Wakorintho 15:23 1stCorinthians 15:23

Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.

1 Wakorintho 15:24 1stCorinthians 15:24

Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

1 Wakorintho 15:25 1stCorinthians 15:25

Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.

1 Wakorintho 15:26 1stCorinthians 15:26

Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

1 Wakorintho 15:27 1stCorinthians 15:27

Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.

1 Wakorintho 15:28 1stCorinthians 15:28

Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

1 Wakorintho 15:29 1stCorinthians 15:29

Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?

1 Wakorintho 15:30 1stCorinthians 15:30

Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa?

1 Wakorintho 15:31 1stCorinthians 15:31

Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku.

1 Wakorintho 15:32 1stCorinthians 15:32

Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa.

1 Wakorintho 15:33 1stCorinthians 15:33

Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

1 Wakorintho 15:34 1stCorinthians 15:34

Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.

1 Wakorintho 15:35 1stCorinthians 15:35

Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?

1 Wakorintho 15:36 1stCorinthians 15:36

Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa;

1 Wakorintho 15:37 1stCorinthians 15:37

nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo;

1 Wakorintho 15:38 1stCorinthians 15:38

lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.

1 Wakorintho 15:39 1stCorinthians 15:39

Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.

1 Wakorintho 15:40 1stCorinthians 15:40

Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.

1 Wakorintho 15:41 1stCorinthians 15:41

Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota.

1 Wakorintho 15:42 1stCorinthians 15:42

Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika;

1 Wakorintho 15:43 1stCorinthians 15:43

hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu;

1 Wakorintho 15:44 1stCorinthians 15:44

hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko.

1 Wakorintho 15:45 1stCorinthians 15:45

Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.

1 Wakorintho 15:46 1stCorinthians 15:46

Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho.

1 Wakorintho 15:47 1stCorinthians 15:47

Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.

1 Wakorintho 15:48 1stCorinthians 15:48

Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.

1 Wakorintho 15:49 1stCorinthians 15:49

Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.

1 Wakorintho 15:50 1stCorinthians 15:50

Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika.

1 Wakorintho 15:51 1stCorinthians 15:51

Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

1 Wakorintho 15:52 1stCorinthians 15:52

kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

1 Wakorintho 15:53 1stCorinthians 15:53

Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.

1 Wakorintho 15:54 1stCorinthians 15:54

Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.

1 Wakorintho 15:55 1stCorinthians 15:55

Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?

1 Wakorintho 15:56 1stCorinthians 15:56

Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.

1 Wakorintho 15:57 1stCorinthians 15:57

Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

1 Wakorintho 15:58 1stCorinthians 15:58

Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.